Jihad Islami: Baadhi ya Waarabu wanafanya njama dhidi ya Quds tukufu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i30518-jihad_islami_baadhi_ya_waarabu_wanafanya_njama_dhidi_ya_quds_tukufu
Msemaji wa harakati ya Jihad Islamu ya Palestina amesema kuwa, Siku ya Kimataifa ya Qud mwaka huu inaadhimishwa huku mji huo mtukufu ukiwa katika hali mbaya sana na baadhi ya nchi za Kiarabu zikifanya njama dhidi ya eneo hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 15, 2017 23:53 UTC
  • Jihad Islami: Baadhi ya Waarabu wanafanya njama dhidi ya Quds tukufu

Msemaji wa harakati ya Jihad Islamu ya Palestina amesema kuwa, Siku ya Kimataifa ya Qud mwaka huu inaadhimishwa huku mji huo mtukufu ukiwa katika hali mbaya sana na baadhi ya nchi za Kiarabu zikifanya njama dhidi ya eneo hilo.

Daud Shihab ambaye ni msemaji wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesema kuwa, baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati na maeneo mengine ya dunia zinashusha chini nafasi ya Quds tukufu na kufadhilisha riwaya ya kubuni ya Wazayuni kuhusu eneo hilo takatifu, suala ambalo limesababisha matatizo yaliyoonekana kwa sasa.

Shihab amesisitiza kwa, Siku ya Kimataifa ya Quds ni jibu madhubuti linalowadhihirishia walimwengu kwamba, Quds ina nafasi isiyoweza kubadilishwa katika itikadi, fikra na nyoyo za waumini.

Msemaji wa Jihad Islami ya Palestina ameongeza kuwa, maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds ni jibu la Umma wa Kiislamu kwa madola ya kibeberu na vibaraka wao ambayo yanataka kuwatwisha watu wengine mamlaka na matakwa yao.

Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Ruhullah Khomeini kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds. Katika siku hiyo wapigania uadilifu kote duniani hushiiki katika maandamano ya kuwatetea wananchi wanaoendelea kudhulumiwa wa Palestina na na mji wa Quds inaokaliwa kwqa mabavu na Israel ambako ndiko kiliko kibla cha kwanza cha Waislamu.