Hofu ya mapinduzi Saudia, watawala wakwepa mkutano wa G20
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i31370-hofu_ya_mapinduzi_saudia_watawala_wakwepa_mkutano_wa_g20
Mfalme na mrithi wa kiti cha ufalme Saudi Arabia wanaripotiwa kukwepa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za G20 huko Hamburg, Ujerumani kwa kuhofia mapinduzi nchini kwao.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jul 05, 2017 10:01 UTC
  • Hofu ya mapinduzi Saudia, watawala wakwepa mkutano wa G20

Mfalme na mrithi wa kiti cha ufalme Saudi Arabia wanaripotiwa kukwepa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za G20 huko Hamburg, Ujerumani kwa kuhofia mapinduzi nchini kwao.

Hayo yamedokezwa na mkosoaji wa utawala wa Aal Saud ambaye ni maarufu kwa jina la Mujtahid, ambaye katika ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa: "Mfalme Salman bin Abdul Aziz wa Saudi Arabia hatashiriki katika kikao cha G20 kwa sababu ya ugonjwa na kuvurugika uwezo wake wa kiakili." Mujtahid ameongeza kuwa: "Naye Mohammad Bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme Saudia, hawezi kuondoka katika nchi kwa kuhofia kupinduliwa na wanawafalme katika ukoo wa Aal Saud."

Mohammad bin Nayef aliyeuzuliwa wadhifa wa mrithi wa kiti cha ufalme Saudia

Hali si shwari tena Saudi Arabia baada ya mfalme Salman wa nchi hiyo hivi karibuni kuchukua hatua ya kushangaza ya kumteua mwanae, Mohammad bin Salman kuchukua cheo cha mrithi wa kiti cha mfalme ambacho kilikuwa kinashikiliwa na Mohammad bin Nayef aliyeuzuliwa na kupokonywa nyadhifa zote alizokuwa nazo.

Hatua hii imekabiliwa na upinzani mkali wa baadhi ndani ya ukoo unaotawala wa Aal Saud huku kukiwa na tetesi za malumbano makubwa ndani ya ukoo huo.