Kuongezeka harakati za kundi la Daesh (ISlS) nchini Pakistan
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i33128-kuongezeka_harakati_za_kundi_la_daesh_(isls)_nchini_pakistan
Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (lSlS) limetangaza kwamba limehusika na mripuko wa bomu katika mji wa Quetta nchini Pakistan.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 14, 2017 03:56 UTC
  • Kuongezeka harakati za kundi la Daesh (ISlS) nchini Pakistan

Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (lSlS) limetangaza kwamba limehusika na mripuko wa bomu katika mji wa Quetta nchini Pakistan.

Mripuko huo ulitokea jioni ya Jumamosi katika eneo la Pishin Stop katika mji huo wa Quetta ambapo kuna jengo ya bunge la kieneo la jimbo la Baloshestan, chuo kidogo cha sheria na hospitali kadhaa. Inaelezwa kuwa, kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuhusika na shambulizi hilo katika hali ambayo viongozi wa kisiasa na kijeshi nchini Pakistan wamekuwa wakikadhibisha habari ya uwepo wa kundi hilo ndani ya taifa hilo. Katika uwanja huo kuna nukta kadhaa za kuchunguza. Kwanza ni kwamba, katika siku za hivi karibuni mashambulizi ya kigaidi nchini Pakistan na Afghanistan yameongezeka sana kiasi cha kuibua wasiwasi mkubwa.

Baadhi ya hujuma za kigaidi katika makazi ya raia

Pili ni kwamba kutokana na kuwepo maelewano kati ya wanachama kadhaa wa makundi ya kigaidi na baadhi ya viongozi wa usalama nchini humo ni suala lililo mbali kwamba Idara ya Upelelezi ya jeshi la Pakistan (lSl) itakuwa haijui habari ya uwepo wa makundi ya kigaidi kama vile Daesh nchini humo.

Nukta ya tatu ni kwamba, baadhi ya makundi ya kigaidi nchini Pakistan yanadai kuwa, hatua ya kundi la Daesh ya kujitangaza kuhusika na hujuma za kigaidi nchini humo ni kielelezo cha kuwepo mahusiano ya makundi ya kigaidi ya ndani na duru za kigeni ambazo zimekuwa zikiratibu mashambulizi hayo. Kuanzisha vita yenye lengo la kuibu tofuti, kushadidisha mpasuko kati ya Pakistan na lndia pamoja na Afghanistan ambazo zinatuhumiwa kuwa zinahusika katika machafuko ya eneo la Quetta, sambamba na kuhatarisha miradi ya kiuchumi ya China katika jimbo la Balochistan, na kadhalika kusafirisha ugaidi kwenda eneo la Asia ya Kati ni miongoni mwa malengo ya magaidi na waungaji wao mkono katika kuzidisha vitendo vya umwagaji damu hususan katika maeneo yenye migogoro nchini Pakistan hasa Quetta.

Magaidi wasiokuwa na utu wakiwa wameripua eneo la mkusanyiko wa watu

Kuhusiana na sula hilo, Kambakhs Nikui mtaalamu wa masuala ya kisiasa wa Afghanistan anasema: "Kundi la Daesh linazidi kuimarika kutokana na misaada ya nchi kubwa za Magharibi na za Kiarabu za eneo la Mashariki ya Kati. Nchi hizo  zinataka kuwatuma wanachama wa kundi hilo hata eneo la Asia ya Kati na nchi nyingine kwa ajili ya kudhamini maslahi yao", mwisho wa kunukuu. Nukta ya kufaa kuzingatia ni hii kwamba, mashambulizi ya kigaidi nchini Pakistan na Afghanistan ambayo kwa kawaida yanawalenga raia wa kawaida, hayana mahusiano yoyote kidini wala kistratijia bali ni mashambulizi ya kipofu ambayo yana lengo tu la kuibua mgogoro na mchafuko katika eneo.

Askari wa Pakistan

Pamoja na hayo ni kwamba, misimamo ya maulama na wanazuoni wa dini ya kulaani jinai hizo inaweza kusaidia kuzuia vijana kujiunga na makundi hayo ambayo yanatenda jinai na kuwazuia kufuata Uwahabi ambao unaenda kinyume na mafundisho asili ya dini ya Uislamu. Pir Muhammad Mulazahi mtaalamu wa masuala ya kisiasa wa mjini Tehran anasema: "Ili kukabiliana na harakati za kigaidi, viongozi wa kidini, shakhsia tofauti na wanasiasa wa Kishia na Kisuni lazima wasimame katika upande mmoja, ambapo sambamba na kulaani mashambulizi ya kigidi, wanatakiwa kuchukua hatu za kuzuia wimbi hilo."

Maulama wa Pakistan ambao wamekuwa mstari wa mbele kulaani ugaidi

Alaa kullihaal, licha ya serikali na jeshi la Pakistan kudai kuwa wamechukua hatua za lazima kwa ajili ya kukabiliana na makundi ya kigaidi nchini humo, hata hivyo kuendelea vitendo vya umwagaji damu hususan katika mji wa Quette ambao hivi karibuni kamanda wa jeshi la ardhini wa jeshi la Pakistani aliahidi kudumisha usalama na amani, kunahesabika kuwa ni kufeli kukubwa kwa jeshi hilo, ambalo linamiliki uwezo wa makombora na silaha za nyuklia ya kijeshi za hali ya juu.