Wanajeshi wa utawala wa Israel washambulia Wapalestina Ukingo wa Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i33640-wanajeshi_wa_utawala_wa_israel_washambulia_wapalestina_ukingo_wa_magharibi
Wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel Ijumaa usiku waliwashambulia Wapalestina na kuwajeruhi 11 kati yao katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 26, 2017 02:27 UTC
  • Wanajeshi wa utawala wa Israel washambulia Wapalestina Ukingo wa Magharibi

Wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel Ijumaa usiku waliwashambulia Wapalestina na kuwajeruhi 11 kati yao katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Taarifa zinasema wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel Ijumaa waliwashambulia na kuwakandamiza Wapalestina hao waliokuwa wakiandamana kupinga ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuyni kusini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Ujenzi wa vitongoji hivyo ni kinyume cha sheria na kanuni za kimataifa.

Utawala wa Kizayuni wa Israel umekitihirisha ujenzi wa vitongoji hivyo vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu kwa lengo la kubadilisha muundo wa kijiografia wa maeneo ya Wapalestina na kuyapa sura ya Kizayuni.

Vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni vilivyojengwa katika ardhi za Palestina

Lengo la utawala haramu wa Israel ni kueneza satwa yake kamili katika ardhi hizo za Palestina zilizoghusubiwa.

Baada ya kuingia madarakani utawala wa Donald Trump nchini Marekani, wakuu wa utawala haramu wa Israel wamepata kiburi zaidi na hivyo kuzidisha kasi ya ujenzi wa vitongoji hivyo vya Wazayuni. Benjamin Netanyahu waziri mkuu wa Israel amemtaja Trump kuwa muungaji mkono imara wa utawala wa Kizayuni.