HAMAS: Katu hatutautambua rasmi utawala haramu wa Israel
Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, harakati hiyo katu haitautambua utawala ghasibu wa Israel ambao umekuwa ukitenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi wa Palestina.
Saleh al-Arouri amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na Kanali ya Televisheni ya al-Alam hapa mjini Tehran na kutangaza kuwa, si tu kwamba, harakati hiyo haitaitambua rasmi Israel bali katu haitalegeza kamba kuhusu haki yake ya kudumisha mapambano dhidi ya utawala huo vamizi.
Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amebainisha kuwa, harakati hiyo imejiandaa kikamilifu kuilinda na kuitetea Gaza na kwamba, iko tayari kukabiliana na uvamizi mpya wa utawala ghasibu wa Israel.
Aidha Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Iran ni nchi ambayo inaamini muqawama na inalitambua jambo hilo kuwa ni haki ya kisheria na kwamba, hiyo ndio njia pekee ya kuzikomboa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na maghasibu Wazayuni.
Saleh al-Arouri amesema pia kuwa, uhusiano wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umo katika hali ya kupanuka wigo wake katika masuala mbalimbali.
Hivi karibuni pia, Usama Hamdan Mkuu wa masuala ya kigeni wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS alisema kuwa, harakati hiyo ina hamu ya kustawisha uhusiano wake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyuga zote