Ripoti: Marekani na Saudi Arabia zimewapa magaidi wa ISIS silaha
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i37629-ripoti_marekani_na_saudi_arabia_zimewapa_magaidi_wa_isis_silaha
Shirika moja la kimataifa limezilaumu tawala za Marekani na Saudi Arabia kuwa zimekuwa zikiwafikishia magaidi wa ISIS silaha kwa siri kupitia makundi ya wapinzania nchini Syria.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 15, 2017 06:42 UTC
  • Magaidi wa Daesh (ISIS)
    Magaidi wa Daesh (ISIS)

Shirika moja la kimataifa limezilaumu tawala za Marekani na Saudi Arabia kuwa zimekuwa zikiwafikishia magaidi wa ISIS silaha kwa siri kupitia makundi ya wapinzania nchini Syria.

Shirika lisilo la kiserikali la Conflict Armament Research (CAR) limesema hayo katika ripoti yake ya jana Alkhamisi na kuongeza kuwa, silaha zilizotolewa na Marekani na Saudi Arabia kwa waasi nchini Syria zilipelekwa moja kwa moja kwa kundi la Daesh (ISIS)

Ripoti hiyo imetolewa baada ya miaka mitatu ya utafiti kwenye maeneo ya kivita nchini Syria ambapo shirika hilo lilichunguza kwa kina silaha zilizotumiwa na kundi la magaidi wakufurishaji wa ISIS.

Kulingana na ripoti ya CAR, inaonekana kwamba Washington na Riyadh zilitoa silaha, "kwa vikosi vya upinzani vya Syria." Kwanza, shirika hili linaeleza kwamba Marekani haikuwa na haki ya kutuma kwa waasi hao silaha zilizopatikana kutoka kwa wauzaji wa Ulaya. Silaha hizo zilinunuliwa hasa nchini Romania na Bulgaria. Silaha hizo zilizotolewa kwa waasi nchini Syria zilianguka mikononi mwa kundi la Daesh ambalo lilizitumia kufanya jinai za kuogofya.. Ripoti hiyo inasema kuwa, hali hiyo "ilipelekea ISIS kupata kiasi kikubwa cha silaha kubwa za kivita."

Magaidi wa ISIS

Hii si mara ya kwanza kutokea tukio kama hilo. Marekani, Ufaransa na Uingereza ziliwahi kutoa silaha kwa vikosi vya upinzani vya Syria wakati vita vilipozuka nchini humo. Kundi la kigaidi la Jabhat al Nusra (lenye mafungamano na al Qaeda) lilichukua silaha hizo siku chache baadaye.

Kwa upande mwengine waasi wa Syria waliopewa mafunzo na CIA nchini Jordan walitoroka kundi hilo la waasi na silaha zao na kujiunga na makundi ya magaidi wakufurishaji. Serikali ya Syria imekuwa ikiituhumu Marekani na waitifaki wake katika eneo hili kuwa ndio wafadhili wakuu wa magenge ya kigaidi nchini humo.