Hizbullah ya Lebanon: Marekani ni adui mkuu wa Waarabu na Waislamu
Mkuu wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, hii leo ulimwengu umefahamu na kudiriki kwamba, dola la Marekani ndio adui mkuu wa Waarabu na Waislamu.
Ibrahim Amin al-Sayyed, amesema kuwa, taifa la Palestina limesimama kishujaa na limejitolea kwa hali na mali katika kukabiliana na utawala vamizi wa Israel na limetetea na kuhami ardhi zake na Quds Tukufun kwa harakati ya Intifadha.
Mkuu wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon amebainisha kwamba, matukio yanayoshuhudiwa huko Palestina yanathibitisha kwamba, baada ya Rais Donald Trump kutoa tangazo la kuitambua Beitul-Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala dhalimu wa Israel ulimwengu umerejea katika njia sahihi na kuonyesha mtazamo wake wa kweli kwamba, Marekani ndiye adui mkuu wa Waarabu, Waislamu, taifa la Palestina na haki zao.
Wakati huo huo, Sayyid Hashim Safiyudden Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, hii leo Ulimwengu wa Kiislamu umefahafamu na kudiriki maana ya maneno ya Imam Ruhullah Khomeini MA mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye alisema kuwa "Marekani ni Shetani Mkubwa".
Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Hizbullah ya Lebanonnm sambamba na kuashiria nafasi ya harakati hiyo nchini Lebanon na katika Mashariki ya Kati kwa ujumla amesema kuwa, Hizbullah sanjari na kulinda hadhi ya kitaifa na kusimama kidete mbele ya mipango michafu na njama za Marekani na Israel katika eneo hili, imeuokoa Umma wa Kiislamu na hatari ya uvamizi wa Israel.