Indhari ya Unicef kuhusu hali mbaya ya watoto nchini Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i41667-indhari_ya_unicef_kuhusu_hali_mbaya_ya_watoto_nchini_syria
Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) umetahadharisha kuhusu hali mbaya inayowakabili watoto huko Syria.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 15, 2018 03:25 UTC
  • Indhari ya Unicef kuhusu hali mbaya ya watoto nchini Syria

Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) umetahadharisha kuhusu hali mbaya inayowakabili watoto huko Syria.

Marixie Mercado Msemaji wa shirika la Unicef ameeleza kuwa vita nchini Syria vimeathiri maisha ya watoto milioni nane na nusu nchini humo. Ameongeza kuwa mwaka jana wa 2017 watoto 910 waliaga dunia kutokana na vita huko Syria. Msemaji huyo wa Unicef ameendelea kubainisha kuwa watoto milioni moja na laki saba wa Syria wamelazimika kuacha shule huku wengine milioni moja na laki tatu wakikabiliwa na hatari ya kuacha shule. 

Marixie Mercado, Msemaji wa shirika la Unicef 

Wakati huo huo Geert Cappelaere Mkurugenzi wa Eneo la Mashariki ya Kati wa Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa asilimia 40 ya wahanga wa mgogoro huko Syria ni watoto. 

Wakati walipoivamia na kuikalia kwa mabavu miji na maeneo mbalimbali huko Syria, magaidi walizigeuza nyumba za raia, maeneo ya umma, magari, baiskeli na hata vifaa vya kuchezea watoto kuwa mitego ya kulipulia mada zao za milipuko; suala linaloashiria kuwa magaidi hao wanamiliki mada nyingi za milipuko na silaha.