Kiongozi wa Kizayuni aliyefananisha Waafrika na nyani akosolewa vikali
Kundi moja la kupambana na ubaguzi limemkosoa vikali kiongozi wa kidini wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuwafaninisha watu weusi wenye asili ya Afrika na nyani.
Kundi hilo linalojiita Anti-Defamation League lenye makao yake mjini New York limesema matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Rabbi Yitzhak Yosef wa Israel ni ya kibaguzi na yasiyokubalika.
Katika taarifa, kundi hilo limesema kuwafafanisha watu wenye asili ya Afrika na nyani ni jambo ambalo halipaswi kufumbiwa macho hata kidogo na ni ubaguzi wa hali ya juu.
Rabbi Yitzhak Yosef ametoa matamshi hayo ya kebehi na kibaguzi licha ya kuwa yeye ni kiongozi wa Mayahudi wenye asili ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika.
Mayahudi wa utawala haramu wa Israel wamekuwa wakionyesha chuki zao za kibaguzi wazi wazi.
Mwishoni mwa mwezi uliopita, maelfu ya wahajiri wa Kiafrika waliandamana mjini Tel Aviv kulaani ubaguzi wanaotendewa na utawala wa Kizayuni wa Israel. Waandamanaji hao Waafrika walikuwa wamebeba mabango yaliyoandikwa "Sisi ni Wanadamu", huku wakilaani ubaguzi wa rangi wanaofanyiwa katika utawala wa Kizayuni wa Israel.