Mamluki wa Saudia raia wa Sudan waendelea kuangamizwa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i43506-mamluki_wa_saudia_raia_wa_sudan_waendelea_kuangamizwa_yemen
Makumi ya mamluki wa Sudan waliokodishwa na Saudi Arabia wameuawa na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen katika eneo la Asir, lililoko katika mpaka wa kusini magharibi mwa Saudia.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 22, 2018 13:56 UTC
  • Mamluki wa Saudia raia wa Sudan waendelea kuangamizwa Yemen

Makumi ya mamluki wa Sudan waliokodishwa na Saudi Arabia wameuawa na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen katika eneo la Asir, lililoko katika mpaka wa kusini magharibi mwa Saudia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Yemen la Saba, mamluki hao wa Saudia raia wa Sudan wameuawa baada ya ngome zao zilizoko eneo la al-Alab kushambuliwa na wanajeshi wa vikosi vya Yemen, ambapo pia idadi kubwa miongoni mwao wamejeruhiwa.

Habari zaidi zinasema kuwa, shehena za silaha za utawala wa Aal-Saud zimenaswa na kuharibiwa katika operesheni hiyo ya ulipizaji kisasi.

Vikosi vya Yemen vilitekeleza mashambulizi hayo jana Jumamosi, siku moja baada ya watu 20 kuuawa katika mashambulizi mapya ya ndege vamizi za Saudi Arabia kusini mwa mkoa wa Taiz, kusini magharibi mwa Yemen.

 

Wanajeshi wa Sudan baada ya kupata kichapo kutoka kwa Ansarullah Yemen

Kadhalika mashambulizi ya ndege za kivita za Saudia Arabia katika makazi ya raia kwenye mikoa miwili ya al Hudaida na Saada ya magharibi na kaskazini mwa Yemen yaliua raia wasiopungua kumi na kujeruhi wengine wengi siku ya Ijumaa.

Mapema mwezi huu, makumi ya mamluki wengine wa Sudan waliangamizwa baada ya msafara wa magari yao kuvamiwa na vikosi vya Yemen, katika mkoa wa Hajjah kaskazini magharibi mwa Yemen.