HAMAS: Mapambano ndio njia pekee ya kuwakomboa mateka wa Kipalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i4426-hamas_mapambano_ndio_njia_pekee_ya_kuwakomboa_mateka_wa_kipalestina
Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, mapambano ndio njia pekee ya kuwakomboa mateka wa Kipalestina walioko katika jela za utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 04, 2016 23:53 UTC
  • HAMAS: Mapambano ndio njia pekee ya kuwakomboa mateka wa Kipalestina

Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, mapambano ndio njia pekee ya kuwakomboa mateka wa Kipalestina walioko katika jela za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ismail Ridhwan amesema hayo katika Kongamano la Mshikamano na Wapalestina na kubainisha kwamba, muda sio mrefu Wapalestina watasherehekea kukombolewa mateka wote wa Kipalestina walioko katika magereza ya utawala haramu wa Israel.

Ismail Ridhwan amewapongeza mateka wote wa Kipalestina kwa kusimama kwao kidete mbele ya hatua za kiuadui za Wazayuni na ameitaka Mamlaka ya Ndani ya Palestina ifanye hima katika kuwakomboa mateka wa Kipalestina wanaokabiliwa na mteso mbalimbali katika jela na korokoro za utawala bandia wa Israel.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, kuna taarifa kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel unataka kuweko mpango wa mabadilishano ya wafungwa baina yake na Wapalestina. Inaelezwa kuwa, wanajeshi kadhaa wa Israel wanashikiliwa mateka na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS.

Ikumbukwe kuwa, Harakati ya HAMAS imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kwamba, mapambano ndio njia pekee ya kukomboa ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni maghasibu.