Ziara ya barani Ulaya ya Netanyahu, na shabaha ya kuivuruga JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i45418-ziara_ya_barani_ulaya_ya_netanyahu_na_shabaha_ya_kuivuruga_jcpoa
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala dhalimu wa Kizayuni ambaye alimchochea rais wa Marekani, Donald Trump, ajitoe katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA hivi sasa ameamua kuzifungia safari nchi za Ulaya kwa ajili ya kuzichochea ili nazo zijitoe kwenye mapatano hayo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 04, 2018 22:35 UTC
  • Ziara ya barani Ulaya ya Netanyahu, na shabaha ya kuivuruga JCPOA

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala dhalimu wa Kizayuni ambaye alimchochea rais wa Marekani, Donald Trump, ajitoe katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA hivi sasa ameamua kuzifungia safari nchi za Ulaya kwa ajili ya kuzichochea ili nazo zijitoe kwenye mapatano hayo.

Jüdische Allgemeine, chombo cha habari cha Baraza Kuu la Mayahudi wa Ujerumaini mjini Berlin kimesema kuwa, lengo la safari ya Netanyahu nchini humo ni kuilaumu Ujerumani kwa msimamo wake wa kuendelea kubakia katika mapatano ya nyuklia ya Iran na pia kufuatilia madai ya Netanyahu ya eti kuweko kambi za kijeshi za Iran nchini Syria. Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni aliwasili jana (Jumatatu) mjini Berlin Ujerumaini na leo (Jumanne) anatarajiwa kuelekea Paris, Ufaransa na baadaye London, Uingereza.

 

Shabaha ya ziara hiyo ya Netanyahu katika nchi tatu za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ambazo zimo kwenye mapatano ya JCPOA ni kuzichochea nchi hizo ili zifuate msimamo ule ule wa Marekani wa kulazimisha kuongezwa vipengee vipya katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA vinginevyo nazo zijitoe katika mapatano hayo ya kimataifa. Kabla ya rais wa Marekani kutangaza kujitoa katika mapatano hayo, Netanyahu alijitokeza mbele ya vyombo vya habari na kuonesha DVD zenye madai yake ya uongo akidai kuwa Iran imeendelea na miradi yake ya nyuklia aliyodai eti ni ya kijeshi hata baada ya kufikiwa mapatano ya JCPOA. Ijapokuwa dunia nzima ilipuuza madai hayo yasiyo na mashiko hasa kwa vile Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki ambao ndiye msimamiaji mkuu wa mapatano ya JCPOA umethibitisha mara 11 kuwa Tehran imeheshimu kikamilifu mapatano hayo, lakini Donald Trump alitumia madai hayo ya Netanyahu kama sehemu ya kisingizio cha kuitoa Marekani katika mapatano ya JCPOA yaliyofikiwa mwaka 2015. 

Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema katika barua aliyowaandikia mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tofauti kwamba: JCPOA ina baraka kamili za azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa mantiki hiyo JCPOA haihusiani tu na nchi zilizofanikisha mapatano hayo, kama ambavyo haitoi ruhusa pia kwa upande wowote kujifanyia inavyotaka kuhusu mapatano hayo kutokana na siasa za ndani ya nchi yake au kutokana na tofauti zake za kisiasa na serikali iliyopita kabla yake.

Kansela wa Ujerumiani, Angela Merkel na Banjemin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala dhalimu wa Israel

 

Alaakullihaal, Marekani ina chuki binafsi na uadui wa kupindukia dhidi ya Iran na imejitoa kwenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA kwa lengo la kuyavuruga tu. Hivi sasa pande zilizobakia kwenye mapatano hayo ni Uingereza, Ufaransa, Ujerumaini, China, Russia na Iran. Baada ya Trump kujitoa katika mapatano hayo, Iran imetoa fursa ndogo tu kwa nchi za Ulaya kuhakikisha zinatoa dhamana ya kweli ya kulinda manufaa ya Iran katika mapatano ya JCPOA wakati Marekani itakaporejesha vikwazo vyake dhidi ya Tehran. Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha wazi wajibu wa kutolewa haraka dhamana hiyo hasa kwa kuzingatia uzoefu hasi uliooneshwa na nchi za Ulaya wa kutoheshimu ahadi zao kwa Iran. Miongoni mwa masharti ya Iran ya kubakia kwake katika mapatano hayo ya JCPOA ni kutoguswa kabisa mradi wake wa makombora na wala ushawishi wa Iran katika eneo hili, na vile vile suala la Iran kununua mafuta linayohahitajiauhusiano wa benki za Ulaya na Iran na wajibu wa nchi za Ulaya kupinga waziwazi vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.

Tehran imesema wazi kuwa haiwezi kutosheka kwa maneno tu ya nchi za Ulaya kuwa zitaheshimu, kuyahifadhi na kuyalinda mapatano ya nyuklia ya JCPOA, bali kitu kinachoweza kuikinaisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni nchi za Ulaya kuonesha kivitendo nia yao njema katika suala hilo.