Apr 08, 2016 03:56 UTC
  • Maonyesho ya jinai za Saudia nchini Yemen

Wananchi wa mji mkuu wa Yemen, Sana'a wamefanya maonyesho ya picha, michoro na mabango yanayoakisi jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa kifalme wa Saudi Arabia dhidi ya raia wa Yemen

Televisheni ya al Mayadeen ya Lebanon imeripoti kuwa, maonyesho hayo yametawaliwa na picha za mauaji na uharibifu mkubwa uliofanywa na Saudi Arabia na washiriki wake katika mashambulizi ya mwaka mmoja sasa dhidi ya Waislamu wa Yemen.

Wayemeni wanasema maonyesho hayo yanayofanyika mjini Sana'a yatawafichulia walimwengu baadhi ya jinai zinazofanywa na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya raia wa nchi hiyo.

Mashambulizi ya Saudia dhidi ya Yemen yameua raia karibu elfu 30 na kujeruhi maelfu ya wengine. Vilevile zaidi ya asilimia 80 ya asasi na miundombinu ya Yemen imeharibiwa katika mashambulizi hayo ya kikatili.

Tags