Wanachama 300 wa Daesh na Teleban wauawa Afghanistan
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46922-wanachama_300_wa_daesh_na_teleban_wauawa_afghanistan
Msemaji wa Gavana wa Mkowa wa Jowzjan, kaskazini mwa Afghanistan amesema kuwa karibu watu 300 wameuawa katika mapigano yaliyoibuka hivi karibuni kati ya wanachama wa kundi la Taleban na Daesh, mkoani hapo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 21, 2018 09:59 UTC
  • Wanachama 300 wa Daesh na Teleban wauawa Afghanistan

Msemaji wa Gavana wa Mkowa wa Jowzjan, kaskazini mwa Afghanistan amesema kuwa karibu watu 300 wameuawa katika mapigano yaliyoibuka hivi karibuni kati ya wanachama wa kundi la Taleban na Daesh, mkoani hapo.

Muhamed Reza Ghafuri, amesema kuwa mapigano kati ya wanachama wa makundi hayo katika wilaya za Darzab na Qush Tepa, yamekuwa na uharibifu mkubwa kati ya pande mbili.

Zabiullah Mujahid, Msemaji wa kundi la Taleban pia sambamba na kuthibitisha kujiri mapigano hayo, amesema kuwa hivi karibuni wapiganaji wa kundi hilo watawaswaga wapiganaji wa kundi la Daesh (ISIS) katoka katika mkoa huo. Kadhalika ofisi ya uratibu wa masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kwamba, kwa mujibu wa tathmini za awali, karibu familia 500 zimelazimika kuyahama makazi yao kutokana na kushtadi mapigano kati ya wanachama wa makundi hayo ya kigaidi.

Mauaji makali yanayoendelea kujiri katika safu ya magaidi hao

Katika miezi ya hivi karibuni na kwa mara kadhaa wanachama wa kundi la Taleban walishambulia miji ya Jowzjan na Faryab kwa lengo la kuidhibiti kutoka mikononi mwa Daesh. Hata hivyo askari wa Marekani waliingilia kati kwa lengo la kuwasaidia magaidi wa kundi la Daesh.

Kundi la Taleban na baadhi ya viongozi wa serikali ya Afghanistan wamekuwa wakiituhumu Marekani kuwa inawaunga mkono wanachama wa genge la Daesh ambalo limehusika na jinai nyingi za kigaidi katika miezi ya hivi karibuni.