Wapalestina wakumbuka ukatili wa Israel huko Deir Yassin
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i4741-wapalestina_wakumbuka_ukatili_wa_israel_huko_deir_yassin
Wapalestina leo wamekumbuka mwaka wa 68 wa mauaji ya raia 270 wa Kipalestina mikononi mwa kundi la kigaidi la Wazayuni kwenye mji wa Deir Yassin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 09, 2016 11:34 UTC
  • Wapalestina wakumbuka ukatili wa Israel huko Deir Yassin

Wapalestina leo wamekumbuka mwaka wa 68 wa mauaji ya raia 270 wa Kipalestina mikononi mwa kundi la kigaidi la Wazayuni kwenye mji wa Deir Yassin katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Hafla imefanyika leo Jumamosi katika kijiji hicho kilichoko magharibi wa mji wa Quds (Jerusalem) na kote katika Ukingo wa Magharibi. Wapalestina walioshiriki kumbukumbu hizo walisisitiza kuhusu kuendeleza mapambano dhidi ya utawala haramu wa Israel unaoendeleza mauaji ya Wapalestina, upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni sambamba na kubomoa nyumba za Wapalestina na dhulma nyingine mbalimbali. Deir Yassin ni nembo ya ukatili wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina. Itakumbukwa kuwa siku kama ya leo miaka 68 iliyopita, utawala ghasibu wa Israel ulifanya mauaji ya kinyama katika kijiji cha Deir Yassin huko magharibi mwa Baitul Muqaddas. Mauaji hayo yalifanyika wakati wa vita vya kwanza vya Waarabu na Israel na yalifanywa na genge la kigaidi la Irgun na utawala wa Kizayuni lililokuwa likiongozwa na waziri mkuu wa zamani wa Israel Menachem Begin. Eneo la Deir Yassin lilikuwa na umuhimu mkubwa kwa Wazayuni kutokana na kuwa katika njia ya Baitul Muqaddas na karibu na pwani. Baada ya kukivamia kijiji cha Deir Yassin, Wazayuni hao waliwaua kinyama wakazi 270 ambao hawakuwa na hatia yoyote. Mauaji hayo yaliwalazimisha Wapalestina wengi wa eneo hilo kukimbia makazi yao kwa kuhofia kukaririwa mauaji kama hayo ya kinyama.