Answarullah: Magaidi ni jeshi la pili la Saudi Arabia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i47517-answarullah_magaidi_ni_jeshi_la_pili_la_saudi_arabia
Muhammad Ali al Houthi, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amelaani taarifa ya kutangazwa uungaji mkono wa kifedha wa Saudia kwa muungano wa kimataifa wa kijeshi wa eti kupambana na Daesh unaoongozwa na Marekani nchini Syria na kusema, magaidi ni jeshi la pili la Riyadh.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 18, 2018 04:25 UTC
  • Answarullah: Magaidi ni jeshi la pili la Saudi Arabia

Muhammad Ali al Houthi, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amelaani taarifa ya kutangazwa uungaji mkono wa kifedha wa Saudia kwa muungano wa kimataifa wa kijeshi wa eti kupambana na Daesh unaoongozwa na Marekani nchini Syria na kusema, magaidi ni jeshi la pili la Riyadh.

Hivi karibuni Saudia ilitoa kiasi cha Dola milioni 100 kwa muungano huo vamizi wa kimataifa unaoongozwa na Marekani eti ulio dhidi ya Daesh nchini Syria. Muhammad Ali al Houthi ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba hatua hiyo ya Saudia ni uungaji mkono wa kimaaawi kwa ajili ya kufunika kushindwa kisaikolojia kwa viongozi wa utawala wa Aal-Saud. Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amesisitiza kwamba kutangazwa uungaji mkono huo wa kifedha wa Saudia kwa muungano huo wa kimataifa, umethibitisha uharibifu wa usalama na uthabiti wa Syria na Yemen unaotekelezwa katika siasa za watawala wa Saudia kama ambavyo pia umeonyesha uwepo wa mgogoro wa kutowaamini washirika wake kwa ajili ya kuleta mabadiliko.

Muhammad Ali al Houthi, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen 

Aidha ameongeza kwamba, hatua hiyo ya Riyadh, ni kukiri kushindwa muungano wa kimataifa wa kijeshi wa eti kupambana na Daesh unaoongozwa na Marekani nchini Syria. Marekani na waitifaki wake kuanzia mwaka 2014,  kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la Daesh (ISIS), na bila ridhaa ya Umoja wa Mataifa wala idhini ya serikali ya Damascus, iliunda muungano huo na kuivamia Syria na Iraq ambapo hadi sasa muungano huo umesababisha mauaji ya maelfu ya raia wa nchi hizo na kupelekea wengine wengi kujeruhiwa.