Waziri wa Israel: Tel Aviv haina uwezo wa kupambana na HAMAS
(last modified Mon, 01 Oct 2018 08:11:06 GMT )
Oct 01, 2018 08:11 UTC
  • Waziri wa Israel: Tel Aviv haina uwezo wa kupambana na HAMAS

Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Utawala Haramu wa Kizayuni amesema kuwa, kile kinachojiri katika Ukanda wa Gaza, kina upande wa usalama na ni matokeo ya siasa za kupenda vita za Avigdor Lieberman, Waziri wa Vita wa Israel.

Naftali Bennett, amesema kuwa Lieberman amekuwa akipuuza usalama wa walowezi wa utawala huo walio karibu na Ukanda wa Gaza. Aidha Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Utawala Haramu wa Kizayuni amekiri kwamba Israel haina uwezo wa kukabiliana na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS. Kwengineko, Jumapili ya jana walowezi wa Kizayuni 440 wakisindikizwa na polisi wa utawala pandikizi wa Israel, walivamia na kuingia msikiti wa al-Aqsa kupitia upande wa 'Babul-Magharibah.'

Naftali Bennett, Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Utawala Haramu wa Kizayuni 

Hujuma hiyo ilifanyika katika hali ambayo, awali askari wa utawala wa Kizayuni waliwatia mbaroni Wapalestina kadhaa wa mji wa Quds wakiwemo wafanyakazi na walinzi wa msikiti wa al-Aqsa, ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu duniani. Wakati huo huo, harakati za kitaifa na Kiislamu za Palestina katika Ukanda wa Gaza kwa kushirikiana na wakazi wa eneo la Ukingo wa Magharibi zimeanzisha mgomo katika kulalamikia sheria ya kibaguzi ya 'Nchi ya Kiyahudi.'

 

Tags