Wazayuni waendelea kuchimba mashimo kusini mwa Msikiti wa Al-Aqswa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i50194-wazayuni_waendelea_kuchimba_mashimo_kusini_mwa_msikiti_wa_al_aqswa
Wazayuni wamekithirisha njama zao dhidi ya msikiti wa al-Aqswa kwa kuendelea kuchimba mashimo na njia za chini kwa chini kuelekea msikiti huo mtakatifu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 15, 2018 23:14 UTC
  • Wazayuni waendelea kuchimba mashimo kusini mwa Msikiti wa Al-Aqswa

Wazayuni wamekithirisha njama zao dhidi ya msikiti wa al-Aqswa kwa kuendelea kuchimba mashimo na njia za chini kwa chini kuelekea msikiti huo mtakatifu.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, hivi sasa Wazayuni wana mpango wa kuchimba njia ya chini kwa chini yenye urefu wa mita 1200 kuanzia kitongoji cha Salwan huko Quds Mashariki inayokaliwa kwa mabavu hadi Msikiti wa al-Aqswa.

Samir al-Ruweidhi mmoja wa wakazi wa Quds amesema kuwa, wakazi wa kitongoji cha Salwan wamegundua shimo kubwa la chini kwa chini la Wazayuni wakati walipokuwa wakibomoa njia ya chini kwa chini katika eneo hilo. Taarifa zaidi zinasema kuwa, shimo hilo la chini kwa chini linafika hadi Msikiti wa al-Aqswa.

Msikiti wa al-Aqswa unaokabiliwa na njama mbalimbali za utawala haramu wa Israel

Itakumbukwa kuwa, tangu utawala dhalimu wa Israel ulipouvamia na kuanza kuukalia kwa mabavu mji mtakatifu wa Quds mwaka 1967 hadi sasa, umekuwa ukichimba mashimo ya chini ya ardhi katika mji huo hasa katika eneo lake la kale na kandokando mwa Msikiti wa Al-Aqsa ili kuwalazimisha Wapalestina wayahame maeneo hayo na kuweza kuyadhibiti maeneo yanayozunguka msikiti huo mtakatifu.

Lengo la utawala vamizi wa Israel la kuchimba mashimo ya njia za chini ya ardhi chini ya Msikiti wa Al-Aqsa ni kufuta nembo na athari za Kiislamu na za kihistoria za taifa la Palestina.