Jan 17, 2019 07:44 UTC
  • Kongamano la kulaani jinai za serikali ya Bahrain lafanyika Beirut

Washiriki wa Kongamano la Kimataifa la kulaani jinai za utawala wa Aal-Khalifa nchini Bahrain wamekosoa kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya ukandamizaji wa serikali ya Manama kwa raia wake.

Kongamano hilo limefanyika katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut kwa ushirikiano na Kituo cha Haki za Binadamu Bahrain, chini ya kaulimbiu inayosema "Miaka 8 ya ukandamizaji Bahrain mkabala wa kimya cha jamii ya kimataifa.'

Kongamano hilo limejadili kwa kina mbinu za kikatili zinazotumiwa na vyombo vya usalama vya utawala wa Aal-Khalfa kwa lengo la kuwawekea mbinyo wanaharakati wa upinzani nchini humo. 

Washiriki wa mkutano huo wamekosoa vikali hatua ya Bahrain ya kuwakamata na kuwafungulia kesi za kidhalimu wanaharakati wanaopigania mabadiliko nchini humo.

Ukatili wa vyombo vya usalama vya Aal-Khalifa kwa wananchi wa Bahrain

Kongamano hilo limefanyika chini ya wiki moja baada ya Kituo cha Haki za Binadamu na Demokrasia nchini Bahrain kutahadharisha kuhusu hali mbaya ya wanaharakati wa kutetea haki za binadamu waliofungwa katika jela za utawala wa Aal Khalifa nchini humo.

Tangu Februari 14, 2011, Bahrain imekuwa uwanja wa maandamano ya amani ya wananchi wanaopigania uhuru na uadilifu na kutaka nchi hiyo iongozwe na utawala uliochaguliwa na wananchi wenyewe; lakini mauaji, hatua kali za ukandamizaji na hata kuwavua uraia wananchi ndilo jibu ambalo utawala wa kifalme wa Aal-Khalifa umekuwa ukitoa kwa matakwa halali ya wananchi hao.

 

Tags