Silaha za Marekani na magaidi wa Israel zapatikana Syria
(last modified Tue, 19 Feb 2019 08:00:00 GMT )
Feb 19, 2019 08:00 UTC
  • Silaha za Marekani na magaidi wa Israel zapatikana Syria

Askari usalama wa Syria wamenasa idadi kubwa ya silaha za Marekani na Israel zinazomilikiwa na magaidi huko Rif-Dimashq.

Silaha hizo ni pamoja na makumi ya maelfu ya bunduki, makombora, vifaa vya mawasiliano n.k ambazo zilikuwa zimefichwa kwenye maghala ya chini ya ardhi. Ripoti zinasema kuwa baadhi ya silaha hizo zinatumiwa na jeshi la Marekani; huku maroketi ya milimita 128 pia yakitajwa kuwa yametoka Israel.

Askari wa Marekani wakiwa Syria

Jeshi la Syria tarehe nne mwezi huu pia lilifanya oparesheni katika kitongoji kimoja kusini magharibi mwa mji mkuu Damascus na kaskazini mwa eneo la Qantira na kunasa silaha kadhaa, dawa na zana za kijeshi zilizoundwa Marekani na Israel. Marekani na utawala haramu wa Kizayuni pamoja na baadhi ya nchi katika eneo ndizo zinazodhamini pakubwa silaha kwa magaidi tangu kuanza mgogoro huko Syria mwaka 2011.