Bouthaina Shaaban: Chanzo cha ugaidi katika eneo ni utawala wa Kizayuni
(last modified Sun, 10 Mar 2019 14:12:32 GMT )
Mar 10, 2019 14:12 UTC
  • Bouthaina Shaaban: Chanzo cha ugaidi katika eneo ni utawala wa Kizayuni

Mshauri wa Masuala ya Kisiasa na Habari wa Rais wa Syria amesema kuwa chanzo cha ugaidi huko Syria, Yemen, Iraq na Libya ni utawala wa Kizayuni.

Bouthaina Shaaban amesema leo kuwa utawala wa Kizayuni umewapatia matibabu magaidi wa kundi la Daesh waliojeruhiwa na kuwaunga mkono. Bi Shaaban amesisitiza kuwa lengo la mwisho la ugaidi ni kuligawa eneo la Mashariki ya Kati na kufanikisha malengo ya Wazayuni hata hivyo njama hizo hazitazaa matunda.

Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel akimjulia hali gaidi wa Daesh katika hospitalini Israel  

 

Mshauri wa Masuala ya Kisiasa na Habari wa Rais Bashar al Assad wa Syria ameendelea kubainisha kuwa kadhia ya Palestina itaendelea kuwa suala la awali la mhimili wa muqawama na kwamba Syria na Palestina zinawasiliana kati yazo. Amesema kuishambulia Syria ni dhahir shahir kuwa ni sawa na kuilenga moja kwa moja kadhia ya Palestina.