Wapalestina waishukuru Iran kwa kuinua uwezo wa kijeshi wa muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i53362-wapalestina_waishukuru_iran_kwa_kuinua_uwezo_wa_kijeshi_wa_muqawama
Msemaji Rasmi wa Brigedi ya Quds, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesema kuwa utumiwaji wa makombora aina ya Badr 3, unaonyesha ustawi wa uwezo katika sekta ya kijeshi ya muqawama wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 09, 2019 00:01 UTC
  • Wapalestina waishukuru Iran kwa kuinua uwezo wa kijeshi wa muqawama

Msemaji Rasmi wa Brigedi ya Quds, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesema kuwa utumiwaji wa makombora aina ya Badr 3, unaonyesha ustawi wa uwezo katika sekta ya kijeshi ya muqawama wa Palestina.

Abu Hamzah amesema kuwa hakuna shaka yoyote kwamba bila ya uungaji mkono kwa muqawama wa Palestina, ukiongozwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ambao haujasimama hata siku moja, basi ustawi wa sekta ya kijeshi ya muqawama usingepata maendeleo hayo.

Wanamuqawama wa Palestina wanaotoa pigo kwa Israel kila wakati licha ya majivuno yake

Aidha Msemaji Rasmi wa Brigedi ya Quds, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amebainisha kwamba katika vita vya hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza, wanamuqawama wamepata ushindi wa kistratijia dhidi ya Wazayuni maghasibu. Wakati huo huo makundi ya muqawama wa Palestina Jumatano ya jana sambamba na kuuonya utawala Kizayuni juu ya kujaribu subira ya Wapalestina, yalitangaza kuwa wapiganaji wa muqawama huo wamejiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na Wazayuni maghasibu. Sambamba na kutupilia mbali mpango wa Marekani wa 'Muamala wa Karne' makundi hayo ya muqawama yamesisitiza kwamba yatasimama imara kukabiliana na njama zote za Washington.