PLO: Marekani inakusudia kubuni mipaka mipya eneo la Asia Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i54390-plo_marekani_inakusudia_kubuni_mipaka_mipya_eneo_la_asia_magharibi
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO, amesema kuwa mkutano wa kiuchumi wa mjini Manama, Bahrain umefeli kufikia malengo yake na kuongeza kuwa Marekani inakusudia kubuni mipaka mipya katika eneo la Asia Magharibi na kuanzisha muungano ulio dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 27, 2019 03:25 UTC
  • PLO: Marekani inakusudia kubuni mipaka mipya eneo la Asia Magharibi

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO, amesema kuwa mkutano wa kiuchumi wa mjini Manama, Bahrain umefeli kufikia malengo yake na kuongeza kuwa Marekani inakusudia kubuni mipaka mipya katika eneo la Asia Magharibi na kuanzisha muungano ulio dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Hanan Ashrawi, ameongeza kwamba katika kujaribu kutenganisha na kuwaangusha Wapalestina, Marekani inatumia njia tofauti zikiwemo za vitisho, kutoa ahadi bandia na vikwazo, na kwamba kuitisha mkutano wa kiuchumi wa mjini Manama kulikuwa na lengo la kuuzawadia utawala haramu wa Kizayuni kutokana na hatua yake ya kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina na pia kuanzisha mrengo wa muungano dhidi ya muqawama. Kwa upande wake Ghazi Dabur, Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina amesema kuwa, kuna haja ya kulindwa umoja wa Wapalestina na mrengo wa muqawama katika kukabiliana na kila aina ya hatua zinazolenga kufanya mapatano, hadi kufikiwa kukombolewa ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Hanan Ashrawi, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO

Amesisitiza kwamba lengo la mpango wa Muamala wa Karne ni kuisambaratisha kabisa Palestina. Itakumbukwa kuwa mji mkuu wa Bahrain, Manama umekuwa mwenyeji wa mkutano wa kiuchumi wa siku mbili katika fremu ya kutekelezwa mpango wa Kimarekani wa Muamala wa Karne uliobuniwa na Marekani na utawala haramu wa Kizayuni. Mpango huo unalenga kuikabidhi nusu ya eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na mji wa Quds kwa utawala haramu wa Israel, na mji wa Abu Dis ndio utakaofanywa mji mkuu wa Palestina badala ya mji wa Quds. Kwa mujibu wa mpango huo, wakimbizi wa Kipalestina wanaoishi katika nchi mbalimbali hawatakuwa na haki ya kurejea katika ardhi zao asilia na Wapalestina watakabidhiwa tu ardhi iliyosalia katika eneo la Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza, suala ambalo limepingwa ndani na nje ya Palestina