Jeshi la Israel lamuua shahidi Mpalestina huko Ghaza
Kijana mmoja Mpalestina mapema leo asubuhi amekufa shahidi baada ya kupigwa risasi na askari wa Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel huko kusini mwa Ukanda wa Ghaza.
Duru za Kizayuni zimedai kuwa, kijana huyo ameuawa shahidi wakati alipokaribia ukuta wa kibaguzi kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza.
Aidha kwa mujibu wa Televisheni ya Al Mayedeen, jeshi la utawala ghasibu wa Kizayuni limetumia mizinga kulenga maeneo kadhaa ya mashariki mwa Beit Hanun kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza mapema leo asubuhi.
Mashambulizi hayo yanajiri wakati ambao, mapema Jumamosi asubuhi, askari wa utawala wa Kizayuni walishambulia eneo la Deir al Balkh kati mwa Ghaza na kuwaua shahidi Wapalestina wanne.
Katika miezi ya hivi karibuni, Wapalestina wameimarisha harakati zao za kupinga utawala wa Kizayuni hasa baada ya baadhi ya nchi kadhaa za Kiarabu zikiongozwa na Saudia kuanzisha mkakati wa kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.