Ndege za kivita za Israel zakiuka anga ya Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i55494-ndege_za_kivita_za_israel_zakiuka_anga_ya_lebanon
Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimeingia kinyume cha sheria katika anga ya Lebanon hatua ambayo inakiuka azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 20, 2019 08:50 UTC
  • Ndege za kivita za Israel zakiuka anga ya Lebanon

Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimeingia kinyume cha sheria katika anga ya Lebanon hatua ambayo inakiuka azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Jeshi la Lebanon limetoa ripoti Jumanne na kusema ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel na pia ndege za kijasusi za utawala huo zimeingia kinyume cha sheria katika anga ya nchi hiyo Jumatatu. Ndege mbili za jeshi la utawala wa Kizayuni zimeonekana katika anga ya Lebanon na maeneo ya Karibu.

Kwa mara kadhaa ndege za kivita na zile za upelelezi za utawala haramu wa Israel zimekuwa zikikiuka haki ya kujitawala ya Lebanon na kuingia katika anga ya nchi hiyo. Kutokana na chokochoko hizo, jeshi la Lebnon limewasilisha ripoti kwa askari wa Umoja wa Mataifa walioko nchini humo, UNIFIL.

Askari wa Jeshi la Lebanon

Azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililotolewa baada ya vita vya siku 33 kati ya harakati ya Hizbullah na Israel mwaka 2006 liliutaka utawala huo bandia kukomesha chokochoko zake dhidi ya Lebanon. Hata hivyo utawala huo khabithi umekuwa ukikiuka azimio hilo kwa kuingia katika maji na anga ya nchi hiyo.