Usalama warejea katika mji mkuu wa Iraq baada ya machafuko
Usalama umerejea katika mji mkuu wa Iraq Baghdad, baada ya machafuko ya siku kadhaa.
Kwa mujibu wa Televisheni ya Al Alam, mapema Ijumaa asubuhi vikosi vya usalama vya Iraq vilikuwa vinalinda doria katika maeneo yote ya Baghdad baada ya waandamanaji kuondoka na hali kurejea kuwa ya kawaida. Utulivu kamili pia umeripotiwa katika eneo la Medani ya Tahrir ambayo ilikuwa kitovu cha maandamano hayo.
Katika siku za hivi karibuni mikoa kadhaa ya Iraq ukiwemo wa Bahgdad, imekuwa ikishuhudia maandamano ya wananchi wanaolalamikia hali mbaya ya maisha, ukosefu wa ajira na ufisadi katika idara za serikali.

Watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa katika maandamano hayo.
Waziri Mkuu wa Iraq Adel Abdul Mahdi, mapema Ijumaa katika mahojiano ya moja kwa moja kwa njia ya televisheni amesisitiza kuwa atafuatilia matakwa halali ya wananchi.
Ushahidi unaonyesho kuwa maandaano hayo ya hivi karibuni nchini Iraq hayakuibuliwa na wananchi wenyewe bali yalichochewa na maadui. Imedokezwa kuwa asilimi 79 ya jumbe zote za Twitter ambazo zimesambazwa kuhusu maandamano ya Iraq zilienezwa na watumizi wa Twitter walioko Saudi Arabia.