Marekani yaongeza misaada ya kijeshi kwa utawala utendao jinai wa Israel
Marekani imeongeza msaada wa kijeshi kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unaendelea kutenda jinai dhidi ya Wapalestina.
Gazeti la Kizayuni la Haaretz limeandika kuwa katika mwaka 2018, Marekani ilichangia asilimia 15 ya bajeti ya Wizara ya Vita ya Utawala wa Kizayuni na kwa msingi huo hivi sasa msaada wa kijeshi wa Marekani kwa utawala huo umefika dola bilioni 3.3.
Ripoti hiyo imebaini kuwa, kwa mujibu wa mapatano yaliyotiwa siani baina ya Iran na Marekani, kuanzia mwaka 2019 hadi 2028, Marekani itaupa utawala wa Israel msaada wa kijeshi wa dola bilioni 3.3 kila mwaka na kwamba kiwango hicho kinaweza kuongezwa hadi asilimia 10.
Gazeti la Haaretz pia limeongeza kuwa, utawala wa Kizayuni utapokea dola bilioni 5 kwa lengo la kuunga mkono miradi ya pamoja na Marekani kwa lengo la kuimarisha uwezo wake wa makombora.
Marekani inaupa msaada wa kijeshi utawala wa Kizayuni katika hali ambayo utawala huo unaendelea kutekeleza jinai dhidi ya taifa la Palestina ikiwa ni pamoja na kulizingira kinyama eneo la Ukanda wa Ghaza.
Wamarekani wengi wanapinga msaada wa kijeshi wa nchi yao kwa utawala wa Kizayuni wa Israel huku wakisisitiza kuwa fedha hizo zinapaswa kutumika katika kuwasaidia Wamarekani masikini.