Jeshi la Marekani linawahamisha magaidi wa ISIS kutoka Syria hadi Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i56759-jeshi_la_marekani_linawahamisha_magaidi_wa_isis_kutoka_syria_hadi_iraq
Jeshi la Marekani linawabeba mamia ya magaidi wakufurishaji wa ISIS (Daesh) kutoka jangwa la al-Jazira kaskazini mashariki mwa mkoa wa Hasakah Syria na kuwaingiza katika nchi jirani ya Iraq.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 21, 2019 04:42 UTC
  • Jeshi la Marekani  linawahamisha magaidi wa ISIS kutoka Syria hadi Iraq

Jeshi la Marekani linawabeba mamia ya magaidi wakufurishaji wa ISIS (Daesh) kutoka jangwa la al-Jazira kaskazini mashariki mwa mkoa wa Hasakah Syria na kuwaingiza katika nchi jirani ya Iraq.

Shirika rasmi la habari la Syria, SANA, limefichua kuwa, wanajeshi wa Marekani wameonoekana wakiwasafarisha magaidi hao na kuwapeleka katika eneo maalumu nchini Iraq. Duru zinadokeza kuwa magaidi wa ISIS wako mafichoni katika kambi ya wakimbizi ya al-Hol ambayo iko karibu na mpaka wa Syria na Iraq na ambayo inasimamiwa na wanamgambo wa Kikurdi wa Syria wanaojulikana kama SDF.

Kwa mujibu wa SANA, kuanzia Oktoba 9, askari wa Marekani wamewasafirisha mamia ya magaidi wa ISIS na jamaa zao kutoka Syria hadi Iraq. Hiyo ni tarehe ambayo Uturuki na wanamgambo waitifaki wake walianzisha oparesheni dhidi ya Wakurdi kaskazini mashariki mwa Syria.

Magaidi wa ISIS

Ripoti hiyo imedokeza kuwa, askari wa Marekani wamegeuza kituo chao kilicho kinyume cha sheria katika mkoa wa Hasakah nchini Syria kuwa mahala pa kuwapa hifadhi magadi wa ISIS na familia zao ambapo wanafika hapo kabla ya kusafirishwa kwa helikopta hadi Iraq.

Miezi ya nyuma pia kulikuwa na ripoti za kuaminika kuwa muungano wa kijeshi wa kimataifa unaoongozwa na Marekani wa eti kupambana na ugaidi umewatorosha viongozi kadhaa ISIS katika eneo la Deir ez-Zor mashariki mwa Syria.

Tangu mwaka 2014, Marekani na waitifaki wake zimeunda muungano wa kijeshi kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi la ISIS lakini bila kibali cha Umoja wa Mataifa wala mashauriano na serikali ya Syria. Muungano huo hadi sasa umeshaua na kumwaga damu za raia chungu nzima wasio na hatia katika nchi za Iraq na Syria.