Marekani na Israel zachochea na kuunga mkono machafuko ya Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57093-marekani_na_israel_zachochea_na_kuunga_mkono_machafuko_ya_iraq
Rais wa Marekani na Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameeleza kufurahishwa na machafuko ya Iraq na kusema wanaunga mkono hali hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 06, 2019 08:05 UTC
  • Marekani na Israel zachochea na kuunga mkono machafuko ya Iraq

Rais wa Marekani na Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameeleza kufurahishwa na machafuko ya Iraq na kusema wanaunga mkono hali hiyo.

Kuanzia tarehe Mosi Okoba Iraq ilikumbwa na maandamano dhidi ya serikali yaliyoendelea kwa siku kadhaa na kuanzia Oktoba 25 yalianza tena na kuendelea hadi sasa. Maandamano hayo yanandaana na ghasia kubwa za mitaani na mauaji ya idadi kubwa ya waandamanaji.  Maandamano ya wananchi wa Iraq ni radiamali sahihi ya kulalamikia ukosefu mkubwa wa ajira, ufisadi na huduma mbovu za kijamii. Pamoja nayo inatpasa kusema kuwa, ghasia za mitaani na njama za kusababisha mapigano kati ya askari usalama na wafanya maandamano ni matukio yanayosimamiwa na kuratibiwa na wapinzani wa mfumo wa kisiasa wa Iraq.

Ghasia na machafuko ya mitaani ya wananchi wa Iraq 
 

Marekani na Israel sambamba na kufurahishwa na machafuko yanayoendelea Iraq, zimeparamia maandamano hayo ya amani ya wananchi na kuyafanya ghasia na machafuko ya mitaani. Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais Donald Trump wa Marekani ameonyesha tena picha mbili za video za tukio la kushambuliwa ubalozi mdogo wa Iran katika mji wa Karbala. Picha hizo awali zilioneshwa katika ukurasa wake wa Twitter wa televisheni ya Iran International inayofadhiliwa na mrithi wa kiti cha Saudi Arabia, Muhammad bin Salman na tovuti ya habari ya Arab News. Wakati huo huo, Yisrael Katz Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Jumapili tarehe Pili mwezi huu aliunga mkono waziwazi matukio yanayojiri Iraq kupitia ukurasa wake wa Twitter na kudai kuwa, Iran inahusika na ghasia nchini humo. Jumbe hizo zinaashiria nukta muhimu kadhaa. Ya kwanza ni kuwa, Marekani na Israel pamoja na mhimili wa Kiarabu ndizo zinazoratibu ghasia hizo za mitaani huko Iraq. Kuhusiana na suala hilo, Qais al Khazali Katibu Mkuu wa Harakati ya Asa'ib Ahlul Haq ya Iraq amesema: "Israel ina nafasi kubwa zaidi kuliko Marekani katika machafuko ya sasa nchini Iraq. Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad) lina maajenti wake katika mikoa kadhaa kaskazini mwa Iraq na hata huko Suleimaniya. Vilevile kuna mtandao wa pamoja wa majasusi wa CIA na MOSSAD katika uwanja wa ndege wa Baghdad. Mossad inawatumia baadhi ya shakhsia wa mirengo potovu iliyofukuzwa na vyama vya kisiasa ili kushadidisha mapigano."

Qais al Khazali, Qais al Khazali Katibu Mkuu wa Harakati ya Asa'ib Ahlul Haq ya Iraq
 

Nukta ya pili ni kwamba, Washington na Tel Aviv zinatumia mirengo iliyopotoka ya Kishia na mabaki ya chama tawala cha zamani cha Iraq cha Baath lengo likiwa ni kuathiri matukio ya Iraq na kubadili matakwa ya kiuchumi ya wananchi wa Iraq na kuwa ya kisiasa.Tatu ni kuwa, Marekani na Israel zinatumia vyombo vyao vya habari na vilevile mitandao ya kijamii kuyafanya maandamano hayo yaonekane kuwa ni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ili kufuatilia malengo yao dhidi ya Iran katika ardhi ya Iraq. Israel, Marekani na mhimili wa Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia kwa upande mmoja haziridhishwi na uhusiano wa karibu kati ya Iran na Iraq. na kwa upande mwingine zinapinga ushawishi na nafasi ya kieneo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.Utawala wa Kizayuni, Marekani na mhimili wa Kiarabu ambazo zimekatishwa tamaa na stratejia yao ya vikwazo na mashinikizo ya juu na kuibua machafuko ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, zinajaribu kila ziwezalo ili kuzisababishia machafuko nchi waitifaki wa Iran katika eneo hili. Kupitia njama na proganda hizo, Israel, Marekani na mhimili wa Kiarabu zna lengo la kuiarifisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa chanzo cha machafuko na kuvuruga uhusiano wa Tehran na waitifaki wake ikiwemo Baghdad.Nukta ya mwisho ni kwamba, wananchi wa Iraq hawajaathiriwa na harakati hizo za Israel, Marekani na Saudi Arabia na wenzake, na kwa kuchoma moto bendera za Israel na Marekani wameonyesha kuwa wanapinga uingiliaji wa aina yoyote wa nchi ajinabi katika masuala ya ndani ya Iraq.