Rais wa Lebanon; Uchunguzi kuhusu ufisadi nchini tayari umeanza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57121-rais_wa_lebanon_uchunguzi_kuhusu_ufisadi_nchini_tayari_umeanza
Rais Michel Aoun wa Lebanon amesema kuwa tayari yamewaslishwa mafailili 17 ya ufisadi kwa ajili ya kuchunguzwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 08, 2019 00:39 UTC
  • Rais wa Lebanon; Uchunguzi kuhusu ufisadi nchini tayari umeanza

Rais Michel Aoun wa Lebanon amesema kuwa tayari yamewaslishwa mafailili 17 ya ufisadi kwa ajili ya kuchunguzwa.

Rais wa Lebanon ameongeza kuwa baadhi ya maafisa wa sasa na wa zamani wa nchi iyo watahojiwa kutokana na kushukiwa katika kesi hizo za ufisadi. Wakati huo huo televisheni ya al Mayadeen imetangaza kuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon Fouad Siniora ameitwa mbele ya Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo Ali Ibrahim. 

Juzi Jumatano ilielezwa kuwa Ali Ibrahim Alhamisi wiki hii alitazamia kupokea maelezo kutoka kwa Fouad Siniora Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon kuhusu namna alivyotumia dola bilioni 11 wakati alipokuwa akishikilia wadhifa huo kati ya mwaka 2006 hadi 2008. 

Fouad Siniora,  Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon anayekabiliwa na tuhuma za ufisadi

Siniora Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon ambaye alikuwa karibu na Harakati ya Machi 14 ametoa radiamali yake kwa suala hilo na kuliambia gazeti la al Sharqul Ausat la Saudia kwamba hatofika katika ofisi ya Ali Ibrahim kutoa maelezo. Dola bilioni 11 zilipotea huko Lebanon kati ya mwaka 2006 hadi 2008; kipindi ambacho Fouad Siniora  alikuwa Waziri Mkuu.