Afisa wa Hizbullah: Marekani inataka kuweka serikali kibaraka Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57145-afisa_wa_hizbullah_marekani_inataka_kuweka_serikali_kibaraka_lebanon
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Utendaji la harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa Marekani inataka kuweka serikali kibaraka huko Lebanon.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 08, 2019 23:44 UTC
  • Afisa wa Hizbullah: Marekani inataka kuweka serikali kibaraka Lebanon

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Utendaji la harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa Marekani inataka kuweka serikali kibaraka huko Lebanon.

Sheikh Ali Damoush amesema kuwa, Marekani na waitifaki wake wanataka kubadili mlingano wa kisiasa nchini Lebanon kwa maslahi yao. Sheikh Damoush amesema, kuundwa serikali huru ni takwa kuu la wananchi na muqawama wa Lebanon na kuongeza kuwa: Marekani inafanya kila iwezalo ili kuigeuza Lebanon na kuwa nchi mbadala kwa ajili ya wakimbizi na kushambulia muqawama na waungaji wake mkono. 

Habari nyingine kutoka Lebanon zinasema kuwa, Rais wa nchi hiyo Michel Aoun amesema kuwa hivi karibuni Bunge litaanza kuchunguza sheria za marekebisho katika sekta mbalimbali. Rais wa Lebanon ameongeza kuwa, zinaafanyika juhudi za kutekeleza marekebisho ya uchumi ya serikali iliyojiuzulu.  

Rais Michel Aoun wa Lebanon
 

Kupunguzwa mishahara ya mawaziri na wabunge kwa asilimia 50, kufutwa akaunti za siri za maafisa serikalini na kutoainishwa tozo jipya la ushuru katika bajeti ya nchi hiyo katika mwaka ujao wa 2020 ni miongoni mwa vipengee vya mpango wa marekebisho ya kiuchumi ya serikali ya Saad Hariri kabala ya kujiuzulu. 

Rais wa Lebanon ameongeza kuwa hadi kufikia sasa wakimbizi wa Syria 390,000 wamerejea nchini kwao kwa awamu tofauti. Lebanon imekumbwa na maandamano ya wananchi wanaolalamikia hali ngumu ya maisha na ufisadi serikalini tangu Oktoba 17 mwaka huu hadi sasa. Waziri Mkuu wa nchi hiyo amelazimika kujiuzulu baada ya siku 13 za maandamano.