Israel imewatia mbaroni mamia ya watoto wa Kipalestina
Utawala wa Kizayuni wa Israel umewatia mbaroni watoto 745 wa Kipalestina wenye chini ya umri wa miaka 18, tangu mwazoni mwa huu hadi sasa.
Hayo ni kwa mujibu wa takwimu mpya za kituo cha kutetea haki za wafungwa cha Palestinian Prisoners Club ambacho kimeongeza kuwa, watoto 200 kati ya 745 wa Kipalestina wamekuwa katika korokoro za utawala huo haramu kwa muda mrefu.
Kituo hicho kimetoa takwimu hizo kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Watoto Duniani ambayo inaadhimishwa hii leo katika sehemu mbalimbali duniani.
Hii ni katika hali ambaoyo, takwimu zilizotolewa na duru za Palestina zinaonyesha kuwa, watoto 61 wa Kipalestina wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi huko Gaza tangu yalipoanza maandamano ya Haki ya Kurejea na Kuvunja Mzingiro Machi 30 mwaka jana.
Kuanzia mwaka 2000 wakati ilipoanza harakati ya Intifadha ya Pili, karibu watoto elfu 2 na 300 wa Kipalestina wameuawa shahidi katika mashambulizi ya askari wa utawala haramu wa Israel.