Google na Facebook zashirikiana na Israel dhidi ya Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57565-google_na_facebook_zashirikiana_na_israel_dhidi_ya_wapalestina
Kamati ya Kuwaunga Mkono Waandishi Habari wa Palestina imetangaza kuwa, makampuni mawili ya Facebook na Google yanashirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel katika njama ya kutaka kuzima sauti za Wapalestina na kuficha jinai ziinazofanywa na utawala huo katili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 28, 2019 23:40 UTC
  • Google na Facebook zashirikiana na Israel dhidi ya Wapalestina

Kamati ya Kuwaunga Mkono Waandishi Habari wa Palestina imetangaza kuwa, makampuni mawili ya Facebook na Google yanashirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel katika njama ya kutaka kuzima sauti za Wapalestina na kuficha jinai ziinazofanywa na utawala huo katili.

Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo imesema kuwa makampuni ya Facebook na Google yamefuta makala elfu 14 za Wapalestina katika mitandao yao katika mwaka uliopita wa 2018 yakishirikiana na utawala wa Kizayuni wa Israel kuzima sauti za Wapalestina.

Taasisi hiyo imelaani kitendo cha makampuni ya Google, Youtube, Twitter na Facebook ya kusalimu amri mbele ya mashinikizo ya utawala ghasibu wa Israel na kukubali kufuta maudhui zinazohusiana na mapambano ya ukombozi wa Palestina.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, makampuni mawili ya Google na Facebook yamefuta asilimia 90 ya maudhui zote zionazohusiana na Palestina kutokana na wito na matakwa ya jeshi la Israel. 

Google na Facebook zinashirikiana na Isarel dhidi ya Wapalestina

Makampuni hayo ya Marekani yamekuwa yakifuta na kuzuia kurasa za watu binafsi, mashirika mbalimbali na hata waandishi habari zinazohusiana na kadhia na mapambano ya uhuru ya Wapalestina na zile zinazofichua na kuanika jinai na uhalifu unaoendelea kufanywa na utawala katili wa Israel dhidi ya taifa linalodhulumiwa la Palestina.