Bashar al Assad: Mustakbali wa Syria unatia matumaini
Rais wa Syria ameitaja Ulaya, Marekani na baadhi ya nyingine nyingine kuwa pande kuu husika katika kuibua machafuko na ukosefu wa amani huko Syria na kusema mustakbali wa nchi yake unatia matumaini.
Akizungumza katika mahojiano na televisheni ya Italia ya Rai News 24 Rais Bashar al Assad ameashiria ushindi mbalimbali wa jeshi la Syria katika vita dhidi ya ugaidi na kueleza kuwa Syria imepata ibra na darsa nyingi kuhusu vita vya sasa nchini humo na akasema anaamini kuwa mustakbali wa nchi yake ni wenye kutia matumaini.

Rais Assad amesema kuwa jeshi la Syria limepata mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya ugadi.
Rais wa Syria aidha amepinga tuhuma za wapinzani wa nchi hiyo kwamba Damascus imetumia silaha za kemikali na kueleza kuwa Syria ilisisitiza tangu kuanza kwa porojo hiyo kuhusu silaha za kemikali kuwa haijatumia aina hiyo ya silaha. Rais Bashar al Assad amezitolea wito nchi ajinabi kuacha kuingilia masuala ya nchi yake na kusema pande zote zinapasa kuheshimu sheria za kimataifa na kuzuia kuzikiuka.
Rais wa Syria vile vile amewakosoa wale wote wanaounga mkono makundi ya kigaidi huko Syria na kusema: Hali ya kisiasa imekuwa tete huko Syria kutokana na kuwepo pande nyingi katika mapigano nchini humo. Amesema na pande hizo zimekusudia kurefusha mapigano hayo na kuyabadili na kuwa vita visivyokuwa na mwisho.