Waziri Mkuu wa Iraq alitaka jeshi kukabiliana na magenge ya wahalifu
-
Adil Abdul-Mahdi
Waziri Mkuu wa Muda wa Iraq amesema kuwa tukio la Medani ya al Wathba limeonesha kuwa, kuna makundi yaliyoanzishwa kwa makusudi yanayoparamia maandamano ya wananchi kwa ajili ya kufanya mauaji na kuzusha hofu na wahka nchini Iraq.
Adil Abdul-Mahdi amesema kuwa, kuna udharura kwa vyombo vya usalama kushika silaha na kulinda maandamano ya amani ya wananchi ili yasitekwe na mirengo ya kisiasa.
Katika mwenedelezo wa mashambulizi ya makundi ya wahalifu yanayofuatana na maandamano ya amani ya wananchi wa Iraq ikiwa ni pamoja na mauaji yanayofanywa na makundi hayo na kuwafyatulia risasi waandamanaji, Akhamisi ya jana mitandao ya kijamii ilionesha picha ya kijana aliyekuwa na umri wa miaka 16 akiwa ametundikwa kwenye mlingoti wa taa kwenye Medani ya al Wathba mjini Baghdad.
Picha ya maiti ya kijana huyo iliyotundikwa kwenye mlingoti wa umeme imeitisa Iraq na kuzusha mjadala mkubwa kuhusiana na makundi ya wahalifu wanaoparamia maandaman ya amani ya wananchi.
Msemaji wa Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Iraq Abdelkarim Khalaf amesema kuwa wahusika wa mauaji hayo ya kutisha watachukuliwa hatu kali za kisheri.