Hakim: Mapinduzi ya Kiislamu yaliibua mlingano mpya katika eneo
(last modified Tue, 11 Feb 2020 04:45:36 GMT )
Feb 11, 2020 04:45 UTC
  • Hakim: Mapinduzi ya Kiislamu yaliibua mlingano mpya katika eneo

Mwenyekiti wa Mrengo wa Kitaifa wa Hikmat nchini Iraq amesema, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyoongozwa na Imam Khomeini MA yameweza kuvunja njama zote za maadui dhidi ya Iran katika kipindi cha miaka 40 iliyopita sambamba na kuibua mlingano mpya katika eneo la Asia Magharibi na dunia nzima kwa ujumla.

Sayyid Ammar Hakim, Mwenyekiti wa Mrengo wa Kitaifa wa Hikmat nchini Iraq aliyasema hayo Jumatatu kwa mnasaba wa mwaka wa 41 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuwadia siku ya arubaini tokea kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mwenyekiti wa Harakati ya Al Hashd al Shaabi ya Iraq. Sayyid Amar Hakim amesema majenerali hawa wawili waliweza kuleta mafanikio yaliyojaa baraka kwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Aidha amesema kuwapoteza majenerali hawa wawili ni hasara kubwa lakini Mapinduzi ya Kiislamu yataendelea na mkondo na stratijia yake na yanaweza kuwalea majenerali wengi.

Mashahidi Luteni Jenerali Qassem Solaimani (kushoto) na Abu Mahdi al Muhandes,

Luteni Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes, wakiwa na wenzao wanane, waliuawa shahidi mapema  Ijumaa 3 Januari katika shambulizi la jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq. Jenerali Soleimani alikuwa safarini nchini Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo.

Mapinduzi ya Kiislamu yalipata ushindi Februari 11 mwaka 1979 baada ya kuangushwa utawala wa kiimla wa mfalme Shah. Februari 11, 2020 inasadifiana na mwaka wa 41 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.

Tags