HAMAS: Umoja wa Muqawama wa Palestina utaushinda 'Muamala wa Karne'
(last modified Wed, 26 Feb 2020 12:53:25 GMT )
Feb 26, 2020 12:53 UTC
  • HAMAS: Umoja wa Muqawama wa Palestina utaushinda 'Muamala wa Karne'

Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ameashiria jibu la wanamapambano wa Palestina dhidi ya mashambulio ya karibuni ya Wazayuni na kusisitiza kuwa: Muqawama utaushinda pia mpango wa Muamala wa Karne.

Salah Al-Bardawil, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Hamas amekieleza kituo cha habari cha Falastinu-Alyaum kuwa muqawama wa Palestina umeonyesha katika mashambulio yake ya karibuni kuwa unao uwezo wa kumfanya adui asite kushambulia, kwa namna ulivyokabiliana na utawala wa Kizayuni.

Al-Bardawil amebainisha kuwa, muqawama wa Palestina umeweza kuiteteresha Israel na kupata ushindi mwingine mpya na kwamba mashambulio ya karibuni ya muqawama dhidi ya Wazayuni ni ujumbe kwa wale wote wanaodhani kuwa wanaweza kuifuta haiba ya taifa la Palestina.

Wanamuqawama wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina

Afisa huyo mwandamizi wa Hamas ameongeza kuwa, kipigo chochote unachopata utawala wa Kizayuni kitatoka kwa taifa zima la Palestina; na wananchi wa Palestina wanaunga mkono muqawama na mikakati yake.

Alfajiri ya kuamkia Jumatatu, utawala wa Kizayuni ulishambulia ngome za brigedi za Sarayal-Quds, tawi la kijeshi la Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina nchini Syria na kuwaua shahidi wanamuqawama wawili wa harakati hiyo. Kufuatia hujuma hiyo, muqawama wa Palestina walijibu jinai hiyo ya utawala haramu wa Israel kwa kuvishambulia kwa makombora vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.../

Tags