Saudia yaamua kupunguza uzalishaji mafuta
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i60515-saudia_yaamua_kupunguza_uzalishaji_mafuta
Saudi Arabia imetangaza kupunguza uzalishaji mafuta kabla hata ya muda uliofikiwa hivi karibuni katika kikao cha Jumuiya ya Nchi Zinazozalisha Mafuta kwa Wingi Duniani (OPEC).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 21, 2020 06:59 UTC
  • Saudia yaamua kupunguza uzalishaji mafuta

Saudi Arabia imetangaza kupunguza uzalishaji mafuta kabla hata ya muda uliofikiwa hivi karibuni katika kikao cha Jumuiya ya Nchi Zinazozalisha Mafuta kwa Wingi Duniani (OPEC).

Katika kikao chao cha 9 cha Mawaziri wa Mafuta na Nishati wa nchi 23 wanachama wa jumuiya hiyo, washiriki walikubaliana kupunguza uzalishaji mafuta kwa karibu mapipa milioni 10 kwa siku kuanzia mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu. Saudi Arabia na wanachama wengine wa Jumuiya ya Nchi Zinazozalisha Mafuta kwa Wingi Duniani (OPEC) wanafikiria kupunguza uzalishaji wao wa mafuta haraka iwezekanavyo, hata bila kusubira hadi mwezi ujao, kama walivyokubaliana katika kikao chao na nchi zingine za Marekani na Russia.

Bei ya mafuta duniani imeporomoka zaidi kutokana na hatua za Saudia

Makubaliano ya kupunguzwa uzalishaji mafuta ndani ya OPEC na washirika wake si tu kwamba hayajapelekea kuongezeka na hatimaye kupatikana uthabiti wa bei ya mafuta katika soko la dunia, bali yamekuwa sababu ya kuendelea kuporomoka kwa bei ya mafuta duniani kinyume na ilivyotarajiwa. Katika uwanja huo Jumatatu ya jana Kevin Kramer, Seneta wa chama cha Republican nchini Marekani ameikosoa vikali Saudi Arabia kwa kuzalisha mafuta zaidi katika soko la dunia, suala ambalo limepelekea kuporomoka zaidi bei ya nishati hiyo.