Wairaqi waandamana kulaana shambulizi la Daesh dhidi ya Hashd al-Sha'abi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i60747-wairaqi_waandamana_kulaana_shambulizi_la_daesh_dhidi_ya_hashd_al_sha'abi
Wananchi wa Iraq wamefanya maandamano katika mji mkuu Baghdad kulaani shambulizi la hivi karibuni la kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) lililoua na kujeruhi makumi ya wanachama wa harakati ya kujitolea wananchi ya Hashdu Sha'abi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 03, 2020 08:09 UTC
  • Wairaqi waandamana kulaana shambulizi la Daesh dhidi ya Hashd al-Sha'abi

Wananchi wa Iraq wamefanya maandamano katika mji mkuu Baghdad kulaani shambulizi la hivi karibuni la kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) lililoua na kujeruhi makumi ya wanachama wa harakati ya kujitolea wananchi ya Hashdu Sha'abi.

Katika maandamano hayo ya jana Jumamosi katika Medani ya Tahrir katikati mwa Baghdad, waandamanaji hao walisikika wakitoa nara za kulilaani genge hilo la ukufurishaji kwa kufanya jinai na ukatili dhidi ya harakati hiyo ya wananchi.

Wanachama 11 harakati ya kujitolea wananchi ya Hashdu Sha'abi waliuawa huku wengine 20 wakijeruhiwa katika shambulizi la kushtukiza la kundi la kigaidi la Daesh katika maeneo ya Makshifiyah na Balad kaskazini mwa Samarra, mkoani Salah al-Din Ijumaa iliyopita

Vikosi vya ulinzi vya Iraq jana Jumamosi vilianzisha operesheni kubwa ya kiusalama dhidi ya mabaki ya Daesh mkoani Salah al-Din, kusini mashariki mwa nchi.

Marekani, muasisi, muungaji mkono mkuu na mfadhili wa ISIS

Shambulizi hilo la ISIS limejiri siku chache baada ya Msemaji wa Mkuu wa Majeshi ya Iraq kusema kuwa, mazungumzo ya jinsi ya kuondoka kikamilifu majeshi ya Marekani katika ardhi ya nchi hiyo yataanza mwezi Juni mwaka huu.

Mwanzoni mwa mwaka huu Bunge la Iraq lilipasisha sheria ya kuwafukuza wanajeshi wote wa Marekani katika ardhi ya nchi hiyo, baada ya jeshi gaidi la Marekani kumuua aliyekuwa kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran Luteni Jenerali Qassem Soleimani akiwa pamoja na kaimu mkuu wa kikosi cha wapiganaji wa kujitolea cha Hashdu Sha'abi Abu Mahdi Al Muhandes karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.