Maelfu waandamana Israel wakitaka Netanyahu ajiuzulu; anatuhumiwa kufanya ufisadi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i62019-maelfu_waandamana_israel_wakitaka_netanyahu_ajiuzulu_anatuhumiwa_kufanya_ufisadi
Maelfu ya watu wamefanya maandamano katika miji mbalimbali ya Israel wakimtaka Waziri Mkuu wa utawala huo haramu, Benjamin Netanyahu ajiuzulu kwa tuhuma za kufanya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 05, 2020 06:22 UTC
  • Maelfu waandamana Israel wakitaka Netanyahu ajiuzulu; anatuhumiwa kufanya ufisadi

Maelfu ya watu wamefanya maandamano katika miji mbalimbali ya Israel wakimtaka Waziri Mkuu wa utawala huo haramu, Benjamin Netanyahu ajiuzulu kwa tuhuma za kufanya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma.

Waandamanaji hao waliokuwa na mabango yenye kaulimbinu na nara za aina tofauti wamemtaka Benjamin Netanyahu ajiuzulu na kuwasilisha malalamiko yao kuhusu faili la ufisadi linalomkabili mwanasiasa huyo. Vilevile wamelalamikia uzembe na kushindwa kwa serikali ya Netanyahu kukabiliana ipasavyo na maambikizi ya virusi vya corona na mgogogoro wa kiuchumi uliosababishwa na virusi hivyo na kupinga mpango wa Israel wa kutaka kutwaa na kughusubu ardhi ya Palestina ya Ukingo wa Magharibi. 

Katika miezi ya karibuni ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel) zimeshuhudia maandamano makubwa ya kupinga ufisadi na siasa za Waziri Mkuu wa utawala huo haramu, Benjamin Netanyahu.

Ilipangwa kuwa Jumatano iliyopita Israel ingetwaa eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuliunganisha na ardhi nyingine za Palestina zlizoghusubiwa, lakini serikali ya Tel Aviv imesitisha uamuzi huo baada ya mashinikizo makubwa ya wanamapambano wa Palestina na upinzani wa jamii ya kimataifa dhidi ya mpango huo ulioungwa mkno na kufadhiliwa na Marekani.