'Israel' inaongoza kwa maambukizi ya corona duniani
-
Benjamin Netanyahu
Mkuu wa kupambana na ugonjwa wa corona au COVID-19 katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) amesema: "Kwa kuzingatia idadi ya watu, Israel inaongoza kwa kuwa maambukizi ya juu zaidi ya corona duniani."
Ronni Gamzu, mkuu wa kupambana na corona Israel aliyasema hayo Alhamisi katika mkutano na waandishi habari na kuongeza kuwa tokea saa nne usiku Jumatano hadi Alhamisi mchana, watu 595 walikuwa wameambukizwa corona kote Israel na wanne miongoni mwao walipoteza maisha.
Wizara ya Afya ya Utawala wa Kizayuni wa Israel nayo pia imetangaza kuwa, walioambukizwa corona katika utawala huo ni 78,514 ambapo miongoni mwao 345 wako katika hali mahututi.
Hii ni katika hali ambayo miji mingi ya Israel imekuwa ikishuhudia maandamano makubwa katika siku za hivi karibuni ambapo watu wanaolalamikia sera mbovu za waziri mkuu Benjamin Netanyahu katika kukabiliana na corona, wanamtaka ajiuzulu.