Marekani yaingiza shehena ya zana za kijeshi mashariki mwa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i66362-marekani_yaingiza_shehena_ya_zana_za_kijeshi_mashariki_mwa_syria
Duru mbalimbali za habari zimearifu kuwa, silaha na zana za kilojistiki za wanajaeshi magaidi wa Marekani zimeonekana zikiingizwa katika maidani ya mafuta huko Koniko kaskazini mashariki mwa Deir Zor.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Feb 01, 2021 23:30 UTC
  • Marekani yaingiza shehena ya zana za kijeshi mashariki mwa Syria

Duru mbalimbali za habari zimearifu kuwa, silaha na zana za kilojistiki za wanajaeshi magaidi wa Marekani zimeonekana zikiingizwa katika maidani ya mafuta huko Koniko kaskazini mashariki mwa Deir Zor.

Shirika la habari la Syria, SANA limeripoti kuwa msafara wa wanajeshi wa Marekani jana Jumatatu uliwasili katika maidani ya mafuta vya Koniko kaskazini mashariki mwa mkoa wa Deir Zor. Msafara huo wa wanajeshi wa Marekani ulikuwa umejizatiti kwa silaha na zana za kilojistiki. 

Zana za kijeshi za Marekani zikielekea katika maidani ya mafuta ya Koniko nchini Syria  

Marekani imetuma zana hizo za kijeshi  huko Deir Zor kwa lengo la kuimarisha uwepo wa wanajeshi wake kinyume cha sheria  maidani hiyo ya mafuta ya Syria na kuendelea kupora maliasili hiyo ya mafuta.

Marekani siku zote inatuma silaha na zana za kilojistiki katika maeneo inayoyakalia kwa mabavu na katika kambi zake za kijeshi ilizoasisi kaskazini mwa Syria kinyume cha sheria. Ni wazi kuwa, Marekani imegeuza maidani ya mafuta, shule na hospitali zilizoko katika maeneo ya mashariki mwa Syria ukiwemo mkoa wa Deir Zor kama kambi zake za kijeshi.  

Katika siku na miezi ya karibuni wanajeshi wa Marekani waliingiza mamia ya magari yao  katika mkoa wa Hasakah kupitia vivuko haramu ili kutumika katika kambi zake za kijeshi na kuyasaidia pia makundi ya kigaidi na taasisi zake vibaraka.