Apr 05, 2021 12:55 UTC
  • Mwanamfalme Hamza
    Mwanamfalme Hamza

Tovuti ya Axios ya Marekani imefichua kuwa, shirika la ujasusi la Israel, MOSSAD, limehusika katika jaribio la mapinduzi lililofanyika nchini Jordan.

Mtandao wa Axios umeandika kuwa, mfanyabiashara wa Israel anayejulikana kwa jina la Roy Shaposhnik ambaye ni afisa wa zamani wa shirika la ujasusi la Israel, MOSSAD, amekuwa akifanya mawasiliano na Mwanamfalme Hamza bin Hussein na kwamba amempa ahadi ya kumtumia ndege kwa siri akiwa chini ya kifungo cha nyumbani na kumhamishia katika nchi moja ya Ulaya.

Mrithi wa zamani wa ufalme wa Jordan Mwanamfalme Hamza ambaye ni ndugu yake Mfalme Abdullah II wa nchi hiyo anashikiliwa katika kifungo cha nyumbani kwa tuhuma ya kupanga jaribio la mapinduzi na kuhatarisha usalama wa taifa.

Tovuti ya Axios imeripoti kuwa mfanyabiashara huyo wa Israel ambayo amekuwa akitoa huduma kwa serikali ya Marekani, amekuwa akiwasiliana na mwanamfalme huyo aliyeko kwenye kifungu cha nyumbani.

Wakati huo huo serikali ya Jordan imetangaza kuwa, Mwanamfalme Hamza bin Hussein, jamaa zake na watu wengine walioko nje ya nchi wamepanga jaribio la mapinduzi yaliyoshindwa dhidi ya Mfalme Abdullah II. Naibu Waziri Mkuu wa Jordan ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiuo Ayman Safadi amesema kuwa, uchunguzi wa awali kuhusu jaribio hilo la mapinduzi umebaini kuwepo uhusiano baina ya watu waliotiwa nguvuni na wapambe wa Mwanamfalme Hamza. 

Mfalme Abdullah II

Mtandao wa Axion umeripoti kuwa masaa machache baada ya matamshi hayo ya Safadi, shirika la habar la Jordan, Ammon, lenye mfungamano ya vyombo vya usalama vya nchi hiyo, limeripoti kuwa, afisa wa zamani wa MOSSAD anayejulikana kwa jina la Roy Shaposhnik amehusika la jaribio hilo. 

Roy Shaposhnik wenye umri wa miaka 41 aliwahi kuwa mwanaharakati katika chama cha Kadima huko Israel akiwa mshauri wa waziri mkuu wa wakati huo, Ehud Olmert. Baadaye alifanya kazi katika kampuni moja ya masuala ya usalama ilikuwa ikimilikiwa na raia wa Marekani kabla ya kuasisi kampuni yake mwenyewe na kuanzisha uhusiano wa kikazi na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. 

Mwanamfalme Hamza na makumi ya watu wengine walitiwa nguvuni Jumamosi usiku kwa madai ya kuhusika na jaribio la mapinduzi ya utawala wa kifalme wa Jordan. 

Tags