HAMAS yautaka utawala wa Saudi Arabia uwaachilie huru mahabusu wa Kipalestina
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameitaka Saudi Arabia iwaachilie huru mahabusu wote Wapalestina inaowashikilia na kufunga faili lao.
Ismail Hania ametoa wito huona kueleza kwamba, ana matumaini kwamba, watawala wa Saudia watatangaza tarehe maalumu ya kusikilizwa kesi ya mahabusu wa Kipalestina na mahakama husika ifanye kikao na kutoa hukumu ya kuwaachilia huru mahabusu wote wa Kipalestina.
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa: Tunasubiria hukumu ya mahakama na tangazo la kuachiliwa huru wafungwa wa Kipalestina walioshikiliwa katika magereza ya Saudi Arabia.
Hukumu ya wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa huko Saudia inatarajiwa kutolewa Jumapili na Alkhamisi za wiki ijayo.
Watawala wa Saudi Arabia na licha ya matakwa ya kila mara ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS), asasi za haki za binaadamu na familia za watu wanaoshikiliwa huko Saudia, bado wamekataa kuwaachilia huru Wapalestina hao.
Tangu mwaka juzi, Saudi Arabia imewatia mbaroni zaidi ya Wapalestina na Wajordan 60 kwa tuhuma zinazohusiana na kuwa wanachama wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS).
Utawala vamizi w Saudia ambao umeendelea kufanya mauaji dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Yemen umekuwa ukiandamwa na ukosoaji mkubwa wa mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu kutokana na kukiuka haki za binadamu nje na ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu.