Sheikh Naeem Qassim: Muqwama wa Lebanon umejiweka tayari kukabiliana na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i7774-sheikh_naeem_qassim_muqwama_wa_lebanon_umejiweka_tayari_kukabiliana_na_israel
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa harakati hiyo ya muqawama iko tayari kikamilifu kukabiliana na vitisho na uvamizi unaoweza kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 25, 2016 03:01 UTC
  • Sheikh Naeem Qassim: Muqwama wa Lebanon umejiweka tayari kukabiliana na Israel

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa harakati hiyo ya muqawama iko tayari kikamilifu kukabiliana na vitisho na uvamizi unaoweza kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sheikh Naeem Qassim, ameyasema hayo mbele ya hadhara ya vijana wa Lebanon kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 16 wa Sikukuu ya Muqawama na kukombolewa eneo la kusini mwa Lebanon kwa kutimuliwa majeshi vamizi ya utawala wa Kizayuni.

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema, Israel inajua kwamba baada ya kipigo ilichopata kwa harakati ya muqawama endapo itafanya uvamizi wowote, muqawama uko katika mazingira mwafaka ya kutoa jibu kwa uvamizi huo.

Ameongeza kuwa kukombolewa kusini mwa Lebanon kutoka kwenye makucha ya uvamizi wa Wazayuni yalikuwa mafanikio makubwa kwa Walebanon.

Tarehe 25 Mei mwaka 2000, majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel yaliyokuwa yamelivamia na kulikalia kwa mabavu eneo la kusini mwa Lebanon yalitimuliwa katika eneo hilo na vikosi vya muqawama, na sehemu kubwa ya ardhi ya nchi hiyo iliyokuwa imevamiwa na majeshi hayo ikakombolewa.

Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasralullah, baadaye leo anatazamiwa kuhutubia maadhimisho yatakayofanyika kwa manasaba huo.../