Jeshi la Yemen latungua droni ya ujasusi yenye silaha ya Saudia
Msemaji wa jeshi la Yemen amesema kuwa jeshi hilo limeitungua droni ya ujasusi yenye slaha ya Saudi Arabia katika anga ya mkoa wa Hajjah huko Yemen.
Licha ya kupita miaka minane tangu muungano vamizi wa Saudia na washirika wake uanzishe vita dhidi ya Yemen, vikosi vya ulinzi na makundi ya kujitolea ya wananchi wa Yemen sambamba ya kuwalinda raia wa nchi hiyo, vimefanikiwa kutoa pigo kubwa kwa muungano huo vamizi na washirika wake.
Si hayo tu bali jeshi la Yemen na makundi ya kujitolea ya wananchi yameweza kushambulia kuzilenga nchi vamizi za Saudia na Imarati ndani ya ardhi za nchi hiyo. Aidha jeshi hilo limepanua uwezo wake wa kisilaha hasa makombora na droni kwa kutegemea nguvu za ndani licha ya Yemen kuzingirwa kwa pande zote kikamilifu.
Brigedia Jenerali Yahya Saree ametweeti kwa kusema: Ndege moja isiyo na rubani (droni) ya ujasusi aina ya CH4 jana ilitunguliwa katika anga ya mkoa wa Hajjah.
Saree ameongeza kuwa, droni hiyo ilitunguliwa kwa kombora la ardhi kwa anga ikiwa katika oparesheni za kijasusi.