Wajordan waandamana kuwaunga mkono Wapalestina waliozingirwa katika kambi ya Shuafat
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i89298-wajordan_waandamana_kuwaunga_mkono_wapalestina_waliozingirwa_katika_kambi_ya_shuafat
Mamia ya wananchi wa Jordan wameandamana wakiunga mkono muqawama na mapambano ya wananchi wa Palestina na kulaaniwa kuzingirwa Wapalestina katika kambi ya wakimbizi ya Shuafat huko Quds Palestina inayokaliwa kwa mabavu
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Oct 15, 2022 04:21 UTC
  • Wajordan waandamana kuwaunga mkono Wapalestina waliozingirwa katika kambi ya Shuafat

Mamia ya wananchi wa Jordan wameandamana wakiunga mkono muqawama na mapambano ya wananchi wa Palestina na kulaaniwa kuzingirwa Wapalestina katika kambi ya wakimbizi ya Shuafat huko Quds Palestina inayokaliwa kwa mabavu

 Wananchi hao wa Jordan ambao waliandamana jana baada ya Swala ya Ijumaa katika mji mkuu wa nchi hiyo Amman wameitaka jamii ya kimataifa kuungana na wananchi wa Palestina wanaoandamwa na madhila ya jeshi la Israel linalotenda jinai kila uchao.

Waandamanaji hao walikuwa wamebeba mabango na maberamu yaliyoandikwa jumbe zisemazo: "Quds inaungua", "Ijumaa ya Simba wa al-Aqswa", Hatutoucha peke yake Msikiti wa al-Aqswa", "Fungueni Mipaka" na "Sisi ni Mashahidi wa Mamilioni ambao Tunaelekea Beitul-Muqaddas".

Aidha huku wakipiga nara dhidi ya utawala ghasibu wa Israel, waandamanaji hao wameitaka serikali ya Jordan kutumia mashinikizo yote kwa ajili ya kuhitimisha uvamizi wa Wazayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa.

 

Katika miezi ya hivi karibuni vitendo vya hujuma na uvamizi wa walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina hususan katika Msikiti wa al-Aqswa vimeongezeka mno.

Kambi ya wakimbizi ya Shuafat imezingirwa kikamilifu na jeshi la Israel tangu mwanajeshi mmoja wa kike wa Israel alipoangamizwa katika eneo hilo.

Hali ya mambo katika siku za karibuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina hususan katika Ukingo wa Magharibi si ya kawaida kabisa, ambapo wanamuqawama wa Kipalestina wakitumia kila nyenzo wamejibu jinai zisizohesabika za Israel; suala ambalo limewaweka Wazayuni maghasibu katika hali ngumu.