-
Mkuu wa Aramco: Kufungwa Lango-Bahari la Hormuz kumesababisha ‘mshtuko mkubwa kwa usambazaji wa mafuta katika historia’
Aug 05, 2026 02:51Mkurugenzi wa kampuni kubwa ya mafuta ya Saudi Arabia ya Aramco ameeleza kuwa kufungwa Lango-Bahari la Hormuz kumesababisha "mshtuko mkubwa zaidi wa usambazaji wa mafuta katika historia," na kwamba masoko ya dunia yamepoteza mapipa ya mafuta zaidi ya bilioni 2.6 tangu kuanza kutekelezwa hatua hiyo.
-
Sheikh Naim Qassim: Mazungumzo ya moja kwa moja ya Lebanon na Israel hayana tija yoyote isipokuwa aibu na fedheha
Aug 04, 2026 10:28Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Lebanon na Israel hayajakuwa na matokeo yoyote isipokuwa aibu na fedheha.
-
Afisa wa Ansarullah: Kauli za Trump kuhusu amani zimetokana na hofu ya nguvu za Iran
Aug 04, 2026 03:04Afisa mwandamizi wa Ansarullah amesema kuwa matamshi ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu amani yanaonyesha wasiwasi wa Marekani juu ya uwezo wa ulinzi wa Iran.
-
Kwa nini shambulio la Saudi Arabia na Marekani dhidi ya Hashd al-Shaabi ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya kujitawala ya Iraq?
Aug 03, 2026 11:09Kikosi cha Hashd al-Shaabi cha Iraq kilitangaza siku chache zilizopita kuwa watu wasiopungua 20 waliuawa na wengine 32 kujeruhiwa katika shambulio la pamoja la kichokozi lililofanywa na Marekani na Saudi Arabia dhidi ya Iraq mapema Jumatano iliyopita.
-
Muqawama wa Palestina watoa onyo baada ya mashambulizi mabaya zaidi ya Israel tangu kusitisha mapigano
Aug 03, 2026 10:10Makundi ya Muqawama ya Palestina yametoa onyo kali baada ya mashambulizi mabaya zaidi ya anga ya Israel tangu kusitisha mapigano Oktoba 2025, yakisema mashambulizi hayo yasiyokoma ni hujuma ya makusudi dhidi ya makubaliano ya kusitisha mapigano na ujumbe kwamba Israel haina nia ya kutimiza majukumu yake.
-
Kiongozi mkuu wa kidini wa Bahrain alaani mataifa ya Kiarabu kwa kutumikia ajenda za Marekani na Israel
Aug 03, 2026 10:08Ayatullah Sheikh Isa Qassim, kiongozi wa jamii ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Bahrain, amezilaani nchi za Kiarabu na Kiislamu za kanda ya Magharibi mwa Asia kwa kuchangia katika njama za Marekani na Israel za kuimarisha migawanyiko katika eneo hilo.
-
Malengo ya Julani katika kuanzisha uadui dhidi ya kundi la Hashd al-Shaabi la Iraq
Aug 03, 2026 08:39Abu Mohammad al-Julani, mtawala wa serikali ya mpito ya Syria, amedai katika matamshi tatanishi kuwa ana wasiwasi kuhusu uwepo wa makundi ya wanamgambo wa Iraq na vikosi vya Hashd al-Shaabi katika maeneo ya mpaka wa nchi hiyo na Iraq.
-
Maandamano makubwa ya kupinga sera zilizofeli za Benjamin Netanyahu
Aug 03, 2026 02:40Wakazi wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Israel wamefanya maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali wakipinga sera za serikali ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ambazo wamezitaja kuwa zimeshindwa.
-
Katika mwezi wa Julai pekee Israel imeua Wapalestina zaidi ya 150 Ghaza
Aug 02, 2026 13:10Wizara ya Afya ya Ghaza imetangaza kuwa, katika mwezi Julai pekee, Wapalestina 152 waliuawa shahidi katika eneo hilo lililowekewa mzingiro, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya vifo vya kila mwezi kuwahi kurekodiwa tangu ulipoanza mwaka huu.
-
Vita vya kinyama vya Israel Ghaza: Miili 40 ya watoto, 38 ya wanawake miongoni mwa iliyotolewa kwenye kifusi
Aug 02, 2026 12:57Shirika la Ulinzi wa Raia la Ghaza limesema, wafanyakazi wake walipata miili na mabaki ya watu 112 kutoka chini ya vifusi vya nyumba zilizoharibiwa na mashambulizi ya kinyama ya jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel katika kitongoji cha Sabra cha Jiji la Ghaza.