-
Yemen yashambulia Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion wa Israel kwa kombora la masafa marefu
May 05, 2025 07:16Jeshi la Yemen limeulenga Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion karibu na Tel Aviv baada ya majaribio kadhaa ya jeshi la Israel kulizuia kushindikana. Kombora hilo lilipenya na kukwepa ngao nne za ulinzi wa anga na kutua katikati ya Uwanja wa Ben Gurion Jumapili, huku mifumo ya Arrow na THAAD ikishindwa kulizuia kombora hilo la hali ya juu.
-
Yemen yatangaza mzingiro kamili wa anga dhidi ya Israel, itaendelea kulenga viwanja vya ndege
May 05, 2025 06:00Vikosi vya Ulinzi vya Yemen vimetangaza kuwa vitaweka mzingiro kamili wa anga dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuendelea kuvilenga mara kwa mara viwanja vya ndege vya utawala huo haramu.
-
Familia za mateka Wazayuni: Njia pekee ya kuwarejesha mateka ni kuipindua serikali ya Netanyahu
May 05, 2025 06:00Familia za mateka Wazayuni wanaoshikiliwa Ghaza zimesema, anachopigania waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu ni kurefusha vita kwa malengo yake ya kisiasa, kwa hiyo njia pekee ya kuwarejesha mateka wao ni kuipindua serikali ya Netanyahu, na kwamba lengo hilo litafikiwa kwa wazayuni wote kumiminika mabarabarani.
-
Iran yakataa madai ya kuhusika katika operesheni za kulipiza kisasi za Yemen
May 05, 2025 02:59Iran imelaani vikali tuhuma za hivi karibuni zilizotolewa na maafisa wa Marekani na Israel kuhusu kuhusika kwake katika operesheni za kulipiza kisasi za Yemen, ikizitaja kuwa “hazina msingi” na “zinapotosha.”
-
Israeli inaiangamiza Gaza kwa njaa huku dunia ikinyamaza: Watoto 290,000 ‘katika hatari ya kifo’
May 05, 2025 02:56Karibu watoto 290,000 wa Kipalestina wako “katika hatari ya kifo” Gaza huku Israel ikiendelea kutumia njaa kama silaha ya vita, maafisa wa Palestina wanasema.
-
"Uvamizi wa Israel Syria hautayaacha salama mataifa ya Kiarabu, Kiislamu"
May 04, 2025 22:53Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina imesema kuwa, uvamizi wa Israel dhidi ya Syria ni hujuma za dhidi ya mataifa yote ya Kiarabu na Kiislamu hususan Palestina, Lebanon na Syria, na kwamba maeneo mengine ya Kiarabu hayatakuwa salama kutokana na chokochoko hizo na matokeo yake.
-
Wanajeshi wawili wa Israel wauawa kwenye mtego katika handaki Gaza
May 04, 2025 08:05Jeshi katili la Israel limeripoti kwamba wanajeshi wake wawili wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa kutokana na mlipuko katika handaki lililowekwa mitego katika jiji la Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
-
Mtaalamu Mkuu wa UN:Maafisa wa EU washtakiwe kwa ushiriki wao katika jinai za kivita za Israel
May 04, 2025 08:04Mtaalamu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina ametoa wito wa kutaka maafisa waandamizi wa Umoja wa Ulaya (EU), akiwemo Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen na Mwakilishi Mkuu wa EU wa Masuala ya Kigeni na Sera ya Usalama Kaja Kallas, wafikishwe mahakamani kwa ushiriki wao katika uhalifu wa kivita unaofanywa na Israel huko Gaza.
-
Mashambulizi dhidi ya Meli ya Uhuru; Jinai nyingine ya Israel
May 04, 2025 06:13Utawala wa Kizayuni wa Israel umefanya jinai nyingine ya kushambulia kwa droni na ndege zisizo na rubani meli za uhuru (Freedom Flotilla) iliyokuwa inapeleka misaada ya kibinadamu kwa wananchi madhlumu wa Ghaza, na hivyo kuzidisha orodha ya jinai za utawala huo katili dhidi ya ubinadamu.
-
Yemen Yapiga marufuku usafirishaji wa mafuta ghafi ya Marekani kupitia Bahari Nyekundu
May 03, 2025 22:58Serikali ya Yemen imetangaza marufuku ya jumla dhidi ya mafuta ghafi ya Marekani, kama jibu kwa mashambulizi yanayoendelea ya Washington kwenye ardhi ya nchi hiyo ya Kiarabu, pamoja na mashambulizi yanayolenga raia na miundombinu ya kiraia.