-
Israel inashinikiza nchi za Afrika kuchukua Wapalestina wa Gaza
Mar 29, 2025 04:21Utawala ghasibu wa Isarel umeelekeza shirika lake la ujasusi la Mossad kutafuta nchi ambazo zitaafiki mpango wa kupokea idadi kubwa ya Wapalestina watakaohamishwa kwa nguvu kutoka Ukanda wa Gaza.
-
Siku ya Quds: Mamilioni ya Wayemen washiriki maandamano ya kuiunga mkono Palestina
Mar 28, 2025 23:43Wananchi wa Yemen jana walijitokeza kwa mamilioni katika maandamano ya kuunga mkono kadhia ya Palestina ikiwa ni katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ambayo huadhimishwa kila mwaka kwa jina la Siku ya Kimataifa ya Quds.
-
Kushadidi maandamano na malalamiko ya kisiasa huko Israel
Mar 28, 2025 22:59Huku maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yakifanyika katika nchi mbalimbali kwa ajili ya kuunga mkono Palestina na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel, mivutano ya kisiasa na hitilafu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu nayo imeongezeka na kupamba moto zaidi.
-
Zainab Nasrullah: Kuwauwa viongozi wa Muqawama hakutadhoofisha mapambano
Mar 28, 2025 08:40Binti wa Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa kuwauwa viongozi wa Muqawama hakutadhoofisha mapambano ya ukombozi.
-
Al Houthi: Mashambulizi ya Marekani hayawezi kubadilisha msimamo wa Yemen
Mar 28, 2025 08:01Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa nchi hiyo ya Kiarabu itaendelea na misimamo yake isioyumba wa kuwahami Wapalestina na mapambano yao halali ya ukombozi bila kujali ukubwa wa mashambulizi ya kijeshi wa Marekani.
-
Kilele cha ukatili wa Israel; Waliouawa shahidi Gaza wapindukia 50,200
Mar 28, 2025 04:00Jeshi katili la Israel ambalo lilianzisha mashambulizi mapya ya anga katika Ukanda wa Gaza mnamo Machi 18, limeendelea kupuuza miito ya jamii ya kimataifa ya kukomesha ukatili wake katika ukanda huo; ambapo mpaka sasa limeshaua shahidi Wapalestina karibu 900 na kujeruhi wengine karibu 2,000.
-
Radiamali ya Hamas kufuatia kuuliwa shahidi "Abdel-Latif al-Qanoua" katika hujuma ya Israel
Mar 27, 2025 22:59Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imeashiria katika taarifa yake kuhusu kuuawa shahidi Abdel-Latif al-Qanoua Msemaji wa harakati hiyo katika shambulio la utawala wa Kizayuni na kutangaza kuwa: "Kuwalenga kwa masambulizi viongozi wa harakati ya Hamas na wasemaji wake kamwe hakuwezi kuvunja irada yetu.
-
Yemen yautwanga kwa makombora utawala wa Kizayuni/sauti za ving'ora zasikika
Mar 27, 2025 22:58Duru za Kizayuni zimearifu kuwa sauti za ving'ora vya hatari vilisikika jana katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kufuatia shambulio la makombora ililotekelewa na jeshi la Yemen.
-
Hamas yataka walimwengu wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono Palestina Siku ya Quds
Mar 27, 2025 07:39Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa mwito wa kuhamasishwa walimwengu kujitokeza kwa wingi katika siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ili kuonyesha mshikamano na Gaza na al-Quds wakati huu ambapo Israel, kwa uungaji mkono wa Marekani, inaendelea na vita vyake vya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina Gaza, mkabala wa kimya cha dunia.
-
Licha ya vizuizi vya Israel Wapalestina 180,000 wamesali Msikiti wa Al-Aqsa mkesha wa Lailatul-Qadr
Mar 27, 2025 02:57Waislamu Wapalestina wapatao 180,000 walisali Sala ya Tarawehe katika Msikiti wa Al-Aqsa mjini Baitul-Muqaddas usiku wa kuamkia leo na kujiandaa kwa mkesha wa mwezi 27 Ramadhani unaokadiriwa kwamba unaweza ukawa ni Lailatul-Qadr, licha ya vizuizi vikali walivyowekewa na utawala wa Kizayuni wa Israel vya kuingia msikitini humo.